Mwanamke mmoja nchini Misri ameamua kukatiza na gauni la harusi mitaani kupinga masimango anayokutana nayo kwa kuchelewa kuolewa.
Samah Hamdi mwenye
miaka 27 alifikia uamuzi huo baada ya kuchoshwa na kashfa kutoka kwa
watu wanaomzunguka ikiwemo familia yake hasa mama yake mzazi ambao
wamekua wakimsema kutokana na kutokua na mume mpaka sasa.
Hamdi
ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya uzamili alisema ameamua kutembea
hivyo mitaani na kamwe hawezi kuacha dhamira yake hiyo ikiwa kama
ishara ya kupinga mila na desturi inayowakandamiza wanawake wasioolewa.
Samah Hamdi akiwa anatafakari jambo huku akiwa amevaa gauni lake la harusi katika moja ya mitaa jijini Cairo
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553