Chama cha ACT-Tanzania kimelitaka Jeshi la Polisi nchini kuwasaka na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wote waliohusika na tukio la mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Masigo wilayani Mlele mkoani Katavi, Christian Kahongo.
Taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa ACT-Tanzania,
Samson Mwigamba, ilieleza kuwa chama hicho kinalaani mauaji hayo ya
kinyama ambayo hayaendani na haki za binadamu.
Alisema
walimkata kichwa na kukitenganisha kabisa na kiwiliwili kisha wakakata
sehemu za siri na baadhi ya viungo vingine vya kichwa wakaanza
kuvikaanga kwenye sufuria.
Alisema huo ulikuwa ni unyama wa ajabu ambao hatujawahi kuushuhudia.
“ACT-Tanzania
tumepoteza shujaa namba moja kati ya mashujaa wanaokiwakilisha chama
chetu kwenye vyombo vya Serikali. Ndiye mshindi wa kwanza kwenye
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kupitia ACT-Tanzania na alipita bila
kupingwa na kuwa wa kwanza kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha
Masigo kupitia ACT-Tanzania.
“Tumepoteza
shujaa kama chama taifa, Mkoa wa Katavi umepoteza shujaa, Jimbo la
Mlele wamepoteza shujaa, vivyo hivyo kwa wanachama wa Kata ya Inyonga na
tawi la Inyonga,” alisema Mwigamba.
Alisema chama kitashiriki msiba huo kwa kuwakilishwa na Mwenyekiti Taifa wa muda pamoja na Katibu wa Ngome ya Vijana Taifa.
“Ikumbukwe
kuwa wauaji hawana rangi, kabila wala vyama, pia hawachagui nani wa
kumuua kama ilivyotokea hivi karibuni kwa askari wetu katika Wilaya ya
Rufiji mkoani Pwani.
“Sisi
ACT-Tanzania tunalaani kwa nguvu zote mauaji haya ya kiongozi wetu si
tu kwa sababu aliyeuawa ni kiongozi wa ACT-Tanzania, bali tutalaani na
kupinga mauaji ya Mtanzania yeyote,” alisema Mwigamba.
Tukio
hilo la mauaji ya kinyama lilitokea Januari 24, mwaka huu ambapo watu
wasiojulikana walivamia nyumbani kwa Christian Kahongo na kumuua kwa
kumkatakata mapanga huku wakimtenganisha kichwa na kiwiliwili,sehemu za siri kisha kuweka kwenye sufuria na kuzipika.