BASI UNAAMBIWA HAWA NDIYO WANAONGOZA KWA KASI KWENYE LIGI YA ENGLAND

eplo speedsters


Unapofikiria wachezaji wanaoongoza kwa kasi wakiwa uwanjani kwenye ligi kuu ya soka nchini England mara moja majina yatakayokujia kichwani ni ya watu kama Raheem Sterling , Gabriel Agbonlahor na Alexis Sanchez
Wachezaji hawa wamezoeleka kuwatisha mabeki kwa kasi yao wakiwa uwanjani jambo ambalo limekuwa msaada mkubwa sana kwa timu zao ambazo zimefaidika kwa mabao yatokanayo na sifa ya wachezaji hawa kuwa na uwezo wa kukimbia kwa kasi ya ajabu .
Kiukweli wana kasi kama ionekanavyo lakini hawajamzidi kiungo Mfaransa wa Newcastle United Mousa Sissoko .
Kiungo huyu wa klabu ya Newcastle United alionekana kuwa na kasi ya ajabu wakati takwmu zilipoonyesha kuwa alikimbia kwa kasi ya kilomita 35.3 kwa saa kwenye mechi kati ya timu yake na Leicester City ambapo Newcastle ilishinda 1-0, kasi ambayo ndio kubwa kuliko wachezaji wote kwa msimu huu kwa mujibu wa takwmu rasmi .
Mousa Sissoko ametajwa kuwa mchezaji mwenye kasi kuliko wote kwenye ligi ya England .
Mousa Sissoko ametajwa kuwa mchezaji mwenye kasi kuliko wote kwenye ligi ya England .
Kwa kawaida Sissoko hajazoeleka kuwa na kasi kubwa na aliwashangaza wengi kwa jinsi takwimu zilivyomuonyesha kuwa na kasi kuwaliko watu kama Wilfred Zaha na wengine wengi .
Wachezaji wengine walioonekana kuwa na kasi kubwa ni kiungo wa West Brom Cristian Gamboa , Eric Dier wa Tottenham na Raheem Sterling wa Liverpool ambao wana kasi ya kukimbia umbali wa kilomita 35 kwa saa .
Alexis Sanchez wa Arsenal ameingia kwenye orodha hii lakini amezidiwa na Gabriel Agbonlahor na Ross Barkley pamoja na Diego Costa wa Chelsea .
Wachezaji wanaoongoza kwa kasi kwenye kila timu ligi ya England 2014-15
MchezajiTimuMpinzani kwenye mechi ya takwimuTareheKasi (kph)
Alexis SánchezArsenalNewcastle United13/12/201434.6
Gabriel AgbonlahorAston VillaSouthampton24/11/201434.8
Marvin SordellBurnleyEverton26/10/201434.0
Diego CostaChelseaLiverpool08/11/201434.7
Wilfried ZahaCrystal PalaceStoke City13/12/201435.2
Ross BarkleyEvertonSwansea City01/11/201434.9
Ahmed ElmohamadyHull CityEverton03/12/201434.6
Marcin WasilewskiLeicester CityQueens Park Rangers29/11/201435.1
Raheem SterlingLiverpoolQueens Park Rangers19/10/201435.0
Sergio AgüeroManchester CityTottenham Hotspur18/10/201434.7
Luke ShawManchester UnitedChelsea26/10/201434.2
Moussa SissokoNewcastle UnitedLeicester City18/10/201435.3
Yun Suk-YoungQueens Park RangersManchester City08/11/201434.7
Nathaniel ClyneSouthamptonStoke City25/10/201434.2
Erik PietersStoke CityWest Bromwich Albion28/12/201434.5
Connor WickhamSunderlandAston Villa28/12/201434.5
Jefferson MonteroSwansea CityEverton01/11/201434.5
Eric DierTottenham HotspurLiverpool31/08/201435.0
Cristian GamboaWest Bromwich AlbionLeicester City01/11/201435.0
Stewart DowningWest Ham UnitedTottenham Hotspur16/08/201435.1
Takwimu hizi zimeonyesha wachezaji wanaoongoza kwa kukimbia umbali mrefu kuliko wote ambapo klabu ya Stoke City imetoa mchezaji anayeongoza ambaye ni Steven N’zonzi ambaye kwenye mechi 20 ameweza kukimbia umbali wa kilomita 227 akiongoza katika takwimu hiyo .
Steve N'zonzi wa Stoke City amekimbia umbali mrefu kuliko wachezaji wote wa ligi ya England baada ya michezo 20.
Steve N’zonzi wa Stoke City amekimbia umbali mrefu kuliko wachezaji wote wa ligi ya England baada ya michezo 20.
Nyuma ya N’zonzi yuko kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas ambaye ukiachilia mbali pasi 14 za mwisho kwa wafungaji wa Chelsea alizotoa ameweza kukimbia umbali wa kilomita 225.3 na anafuatiwa na Cristian Eriksen wa Tottenham Hotspurs ambaye amekimbia umbali wa kilomita 222 umbali ambao ni sawa na mbio tano tofauti za marathon.
Jina la Robin Van Persie limetokea kwenye orodha hii katika hali ambayo itashangaza wengi akiwa amecheza jumla ya mechi 13 pekee ambazo amemaliza dakika 90 ambapo ameweza kukimbia umbali wa kilomita 187.1 na amewazidi Yaya Toure wa Manchester City na Paul Konchesky wa Leicester City ambao wamekimbia umbali wa kilomita 179.7 na 173.1 katika mpangilio .
Wachezaji wanaoongoza kwa kukimbia umbali mrefu ligi ya England 2014-15
MchezajiTimuUmbali aliokimbia (km)
Mathieu FlaminiArsenal191.0
Aly CissokhoAston Villa190.4
George BoydBurnley213.2
Cesc FàbregasChelsea225.3
Joel WardCrystal Palace205.3
Gareth BarryEverton198.2
Jake LivermoreHull City218.2
Paul KoncheskyLeicester City173.1
Jordan HendersonLiverpool204.8
Yaya TouréManchester City179.7
Robin van PersieManchester United187.1
Jack ColbackNewcastle United221.4
Steven CaulkerQueens Park Rangers187.4
Graziano PellèSouthampton199.8
Steven N’ZonziStoke City227.1
Sebastian LarssonSunderland209.1
Ki Sung-YuengSwansea City220.8
Christian EriksenTottenham Hotspur222.8
Craig GardnerWest Bromwich Albion196.2
Aaron CresswellWest Ham United211.5

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post