AUAWA KWA KUKATWA PANGA BAADA YA KUIBA SUPU YA KAKA YAKE

 
Hii inatoka Nigeria, Sunday Osemwekhe alifikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji na amekubali kwamba alifanya kosa hilo, lakini chanzo cha ugomvi wao ilikuwa shutuma alizompa kaka yake kwamba alimuibia supu.


Ugomvi ukaenda mbali zaidi, Osemwekhe aliamua kuchukua panga na kumjeruhi kaka yake huyo sehemu mbalimbali za mwili, ambapo baada ya kufikishwa Hospitali alifariki kutokana na majeraha makubwa.

Uchunguzi wa Polisi Nigeria umeonyesha kuwa mtuhumiwa alishikwa na hasira baada ya kuangalia supu yake aliyoiacha kwenye sufuria ya supu na kugundua haikuwa kama alivyoiacha, mzozo ukaanza kati yake na kaka yake, hasira zilipozidi Osemwekhe alichukua panga na kumpiga kaka yake na kumsababishia majeraha makubwa.


Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post