ANGALIA PICHA-MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI ALIVYOPATA AJALI ENEO LA MLIMA KITONGA
Sunday, January 11, 2015
Mbunge
wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi akifanya mawasiliano kwa
ndugu na jamaa mara baada ya kupata ajali mbaya na kunusurika kifo,ajali
hiyo imetokea eneo la Mlima Kitonga Mkoani Iringa jana.
Mbunge wa Mbeya mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi almaarufu 'Sugu',
amenusurika kufa katika ajali iliyotokea eneo la mlima Kitonga mkoani
Iringa wakati akitokea jimboni kwake kurudi Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tumain
Makene, jana jioni aslisema kuwa, Mbilinyi alipata ajali
hiyo Kitonga baada ya kumaliza ziara mjini Mbeya kuwashukuru wananchi
baada ya ushindi uliopatikana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa
uliomalizika mwaka jana.
Alisema baada ya kufika eneo hilo walipata ajali na kusababisha gari
aina ya Land Cruiser alikuwa amepanda kupinduka na kusababisha kupata
majereha.
Kitonga ni mlima unaotisha wenye bonde upande wa kulia na kushoto na endapo gari linaserereka linatumbukia korongoni.
Makene alisema ndani ya gari hilo walikuwamo abiria wengine ambao
kadhalika wamepata majeraha na kwamba hali zao zinaendelea vizuri.
Mr. Sugu akiwa Hospitali.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi (watatu kushoto) akizungumza namna hali ilivyokuwa mpaka kupata ajali hiyo.
Gari hiyo inavyoonekana.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin