WAKURUGENZI 6 WAANGUKIA PUA KISA KUBORONGA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Serikali imetengua uteuzi wa Wakurugenzi sita wa Halmashauri, na kuwasimamisha kazi wengine watano kupisha uchunguzi, kutokana na kubainika kuchangia kuvurugika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika tarehe 14, mwezi huu.

Akitangaza hatua hiyo kufuatia ripoti iliyoibua madudu yaliyofanyika katika uchaguzi huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Hawa Ghasia amesema uamuzi huo pia umeridhiwa na Rais Jakaya Kikwete.

Mhe. Ghasia amewataja halmashauri ambazo wakurugenzi hao waliotenguliwa uteuzi wao kuwa ni za Mkuranga, Kaliuwa, Kasulu, Serengeti, Sengerema na Bunda, waliosimamishwa kazi ni wakurugenzi wa Hanang', Mbulu, Ulanga, Kwimba pamoja na wa Manispaa ya Sumbawanga.


Waziri Ghasia amesema kuwa Wakurugenzi wengine watatu wamepewa onyo kali, ambao ni wa Rombo, Busege na Muheza na wengine watatu wakipewa onyo la kawaida, wakurugenzi hao ni wa Manispaa Ilala, Hai na Mvomero.


Mtandao Huu Unakujali,Ni Wako!! Tunataka Tukutumie Habari zetu Zote Mara Tu Tunapozipandisha Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa Sasa Hivi ><<VITUKO>>,"MAPENZI",<<HABARI MSETO>>MAGAZETI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527