UTAFITI JUU YA ATHARI YA CHUMVI KWA BINADAMU


o-SALT-SHAKER-facebook
Moja ya vitu ambavyo vimekuwa muhimu kwenye chakula cha mwanadamu ni chumvi ambayo hutumika kuongeza ladha ya chakula ambacho hutumika mezani, umuhimu wa kiungo hiki umefikia hatua ya waswahili kuibatiza chumvi jina la utani ambalo ni Mkuu Wa Jiko, kiungo hiki kinaweza kuwa na madhara pale ambapo inatumika kuliko kawaida na madhara hayo ni kwa afya ya mtumiaji .


Je chumvi ni mbaya kwa Afya yako?
Mwili wa mwanadamu unahitaji chumvi kwa kiwango fulani kwani inasaidia kuongeza madini ambayo mwili wako unayahitaji hatari ni pale unapokula chumvi nyingi kuliko kiwango ambacho mwili wako unahitaji.

Imegundulika kuwa chumvi husababisha matatizo ya shinikizo la damu hali ambayo inaweza ikaongeza uwezekano wa mtu kupata matatizo ya shambulio la moyo pamoja na hatari nyingine za magonjwa ya moyo, inashauriwa utumiaji wa chumvi kwa kiwango cha chini ili kuepukana na matatizo haya.

Je kiasi gani cha chumvi kinazidi kiwango cha kawaida?

Hupaswi kula zaidi ya gramu tano za chumvi kwa siku, hii ni sawa na kijiko kimoja cha chai ambacho kina ujazo wa miligram 5, inajumuisha chumvi ambayo unaongeza ukiwa unapika jikoni, chumvi unayoongeza mezani wakati wa kula na ile chumvi ambayo inapatikana kwenye chakula kiasili hii ni kwa sababu kuna vyakula ambavyo ndani yake kuna chumvi hata kama havina ladha ya chumvi kama vile mikate, Sausage na nyama za kusaga, supu ya kutengenezwa kiwandani, vyakula vya nafaka ambavyo hutumika kwenye kifungua kinywa (breakfast) na hata baadhi ya biskuti.

Je tunatumia chumvi nyingi kuliko kawaida?
Waafrika wengi huwa na kasumba ya utumiaji wa chumvi kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida na hii imezoeleka sana kuanzia majumbani mpaka mahotelini.

Ni rahisi sana kutumia chumvi nyingi kuliko kawaida wakati wa milo ya kila siku.

Nusu ya chumvi ambayo hutumiwa na watu ni chumvi inayopatikana kwenye vyakula hasa vile vya kutengenezwa viwandani ambayo huwekwa wakati wa utengenezaji wa vyakula hivi huko huko viwandani ili kuvifanya vikae kwa muda mrefu, nusu nyingine ni ile ambayo ambayo huongezwa jikoni na ile ambayo watu huongeza mezani wakati wa kula ili kukoleza ladha ya chakula husika.
Salt_Farmers_-_Pak_Thale-edit1
Nini kinatengeneza chumvi?

Chumvi inatengenezwa na vitu viwili ambavyo ni sodium na chloride, sodium ni sehemu ya chumvi ambayo ambayo huongeza presha ya damu au kwa lugha inayoeleweka zaidi huongeza shinikizo au msukumo wa damu hasa pale unapotumia chumvi nyingi kuliko kiwango cha kawaida, taarifa zinaoandikwa kwenye vihifadhi vya vyakula hasa vile ambavyo vinatengenezwa viwandani huonyesha kiwango cha madini ya sodium ambayo yametumika kwenye chumvi, kijiko kimoja cha chai mara nyingi huwa kina miligramu 2000 za sodium.

Ni jinsi gani tunaweza kutumia kiwango cha chini cha chumvi kwenye vyakula ?

Haiwezekani kupunguza kiwango cha chumvi ndani ya siku moja au ghafla , mabadiliko yanapaswa kufanyika hatua moja baada ya nyingine .

Muhimu ni kujizoesha hisia ya kudhani kuwa chakula kina ladha hata pale ambapo chumvi haijakolea
Kama una kawaida ya kuongeza chumvi nyingi mezani hatua ya kwanza ni kuondoa kile kikopo kidogo cha chumvi mezani hasa wakati wa chakula , hii ni kwa sababu unapaswa kukumbuka kuwa kama ulishaongeza chumvi tangu jikoni hauna sababu ya kuongeza nyingine mezani .

Jaribu pia kupunguza kiwango cha chumvi unachoongeza wakati wa mapishi yako, unapaswa kuonja wakati ukiwa unapika ili kuepuka kuongeza kiwango cha chumvi  ambcho kinaweza kuwa hatari kwa Afya yako, kama chakula chako kina viungo ambavyo ndani yake kuna chumvi ya asili hupaswi kuongeza chumvi nyingine juu yake.

Katika tafiti zilizofanyika hivi karibuni imefahamika kuwa kuna baadhi ya vitu vinavyoweza kutumika kama chuimvi ambavyo havna madhara sawa na ya chumvi kwenye mwili wa mwanadamu na mojawapo ni limao pamoja na ndimu.

Kiungo kingine kinachoweza kuchukua nafasi ya chumvi kwenye chakula chako ni mdalasini .
salt
Unataka kujua vyakula visivyo na chumvi nyingi?
Vyakula ambavyo havijatengenezwa kiwandani kwa maana ya vyakula halisi mara nyingi huwa havina chumvi nyingi na hii inamaanisha kuwa unapaswa kuchagua vyakula vya asili kuliko vile ambavyo vimetengenezwa viwandani.


Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527