TAARIFA KAMILI KUHUSU JAMAA ALIYEUAWA KWA KUKATWA JEMBE AKISHANGILIA USHINDI WA CHADEMA HUKO KAHAMA


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha
Mwanamme mmoja aliyefahamika kwa jina la Simeo Isaka (42),mkazi wa kijiji cha Ngokolo kata ya Bukomela tarafa ya Mweli  wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, ameuawa kwa kukatwa na jembe kichwani wakati akishangilia matokeo ya ushindi wa mgombea wake kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa  Shinyanga Justus Kamugisha, alisema tukio hilo limetokea Desemba 15 majira ya saa saba usiku wakati mwanamme akishangilia matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kamanda Kamugisha alisema, marehemu huyo alikuwa  akishangilia ushindi wa mgombea wa Chama Cha Demokrsia na Maendeleo (Chadema), ngazi ya mwenyekiti wa kijiji cha Ngokolo kata ya Bukomela wilayani Kahama.

Kamanda Kamugisha alisema wakati Simeo Isaka akishangilia ushindi huo  ghafla alivamiwa na watu watatu wasiojulikana  kisha kumkata jembe kichwani, na kisha kukimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama ambako alipoteza maisha.

Kamanda  Kamugisha alisema jeshi la polisi linafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo na juhudi za kuwasaka na kuwakamata watuhumiwa wa tukio hilo zinaendelea ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Na Kadama Malunde-Shinyanga


Mtandao Huu Unakujali,Ni Wako!! Tunataka Tukutumie Habari zetu Zote Mara Tu Tunapozipandisha Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa Sasa Hivi ><<VITUKO>>,"MAPENZI",<<HABARI MSETO>>MAGAZETI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527