Majanga ya Mwisho wa Mwaka!! MREMBO AJIRUSHA BAHARINI KWENYE KIVUKO


 
Mrembo mmoja amejirusha baharini katika kivuko cha ferry mapema leo adhuhuri wakati akiwa amepanda kivuko/ferry ya MV Harambee kutoka upande wa Mombasa Kisiwani kuelekea Likoni.


Msichana huyo mwenye umri kati ya miaka 20 na 25 amejirusha kutoka eneo la juu ya Kivuko wakati fery/kivuko  ikiwa katikakati ya bahari ikielekea ufukweni.

Wapiga mbizi wa shirika la Kenya ferry wamejaribu kuokoa maisha yake baada maji kumzidi kutokana na mawimbi makali na akafanyiwa huduma ya kwanza na hatimaye kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Likoni.

 Kwa sasa anapokea matibabu katika hospitali moja mjini Mombasa.

Kulingana na afisa wa uhusiano mwema wa shirika la Kenya Ferry Harun Mutiso amesema kwamba maafisa wa polisi wanachunguza kilichopelekea msichana huyo kutaka kutoa uhai wake.

Hata hivyo kulingana na walioshuhudia ni kwamba wanadada huyo alionekana mtulivu na hakuna aliyetarajia kwamba anaweza jirusha kutoka eneo la juu ya Ferry hadi ndani ya bahari.

Haya yanajiri siku moja baada ya mwanadada mmoja kutoka mtaa wa Mbuzi huko Likoni kumtumia rafiki yake wa kiume ujumbe mfupi kutumia simu ya rununu kwamba atajinyonga kutokana na hali ya maisha kuzidi kuwa ngumu kwake.

 via>>http://www.radiorahma.co.ke

Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527