ANGALIA PICHA MAFURIKO LEO JIJINI DAR ES SALAAM


MVUA ILIYONYESHA LEO JIJINI DAR ES SALAAM IMEZUA BALAA


CHENI ZINAONDOKA NA MAJI

Mvua zilizonyesha kwa muda mfupi katika jiji la dar es Salaam zimesababisha mafuriko katika maeneo ya katikati ya jiji na kusababisha baadhi ya maduka kufungwa na magari kuzimika barabarani kutokana na kuingiwa na maji kulikotokana na tatizo sugu la miundombunu ya maji taka.

Mwandishi wa Malunde1 blog ametembelea katika maeneo mbalimbali ya jiji hapo katika makutano ya barabara ya Morogoro na Bibi titi imeshuhudiwa idadi kubwa ya maduka kufungwa kutokana na hofu ya kuingiliwa na maji yaliyokuwa yamefurika barabarani ambapo baadhi ya madereva wakilazimika kusukuma magari yao baada ya kuziba kutokana na kuingia maji huku watembea kwa wakilazika kupita kwenye maji hali inayoweza kuhatarisha afya zao. 
Wakizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wameitaka serikali kutenga fedha na kuweka mikakati maalumu ili kuondoa kero sugu ya tatizo la miundombinu ya maji taka katika jiji la Dar es Salaam.
Mwandishi wa blog hii amepita katika eneo la Jangwani na kukuta eneo maalumu ya ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi yaendayo haraka likiwa limezungukwa maji ambapo baadhi ya wananchi wanaoishi maeneo hayo wameitaadharisha serikali mradi huo hautaweza kufanya kazi kama inavyokusudiwa hususani wakati wa mvua bila kuongeza kina cha daraja la mto msimbazi ili kuwezesha maji mengi kuelekea baharini.


Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527