MAJAMBAZI YANYONGA MWANAFUNZI KWA KITANDA ALIYEPIGA KELELE YALIPOVAMIA NYUMBA

Watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevunja nyumba na kupora mali mbalimbali kisha kumnyonga mwanafunzi Isihaka Beda wa darasa la saba shule ya msingi Jitegemee iliyopo makao makuu ya wilaya ya Handeni hatua ambayo imesababisha majonzi makubwa kwa wakazi wa wilaya hiyo.

Vilio vya wakazi wa wilaya ya Handeni vilitawala kufuatia watu wasiojulikana kuvunja nyumba ya mkazi mmoja Abida Zubeir wa eneo la Kivesa lililopo makao makuu ya wilaya ya Handeni ambapo wanadaiwa kuvunja na kuiba TV, Deki, Godoro na vifaa vingine mbalimbali kisha kumnyonga mwanafunzi beda kwa kutumia mti wa kitanda cha miti wakati alipokuwa akipiga mayowe.

Kufuatia hatua hiyo baadhi ya makundi ya wazee na viongozi wa mitaa wa wilaya ya Handeni wameiomba serikali kuhakikisha wanawatumia baadhi ya vijana kusaidiana kufichua wahalifu ambao wanaishi nao katika jamii ili kupunguza kasi ya vitendo vya mauaji ya kutisha yanayotishia usalama wa wananchi.

Kamanda wa polisi mkoani Tanga naibu kamishna wa jeshi la polisi Frasser Kashai amethibitisha kutokea kwa tukio na amewaomba wananchi wa wilaya ya Handeni na mkoa wa Tanga kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuhakikisha kuwa vitendo hivyo vinakomeshwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527