UPEPO WADAIWA KUPEPERUSHA KURA ZA WAGOMBEA SHINYANGA VIJIJINI,UCHAGUZI WARUDIWA


Mtandao wa Malunde1 blog umeambiwa kuwa sababu kubwa iliyosababisha kurudiwa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa katika kijiji cha Bubale kata ya Masengwa wilaya ya Shinyanga Vijijini uliokuwa unafanyika Desemba 14,2014 na badala yake kufanyika Desemba 16 ni kwamba wakati zoezi la kupiga kura linaendelea ulitokea upepo wa ajabu uliobeba box la kura za wagombea.

Box la kura zilizopeperushwa na upepo ni lile la wagombea wa uenyekiti wa kijiji cha Bubale.

Mashuhuda wakiwemo wasimamizi wa uchaguzi huo wameiambia Malunde1 blog kuwa wakati zoezi la uchaguzi ghafla ulitokea upepo na kubeba box la kura kisha box hilo kujibamiza kwenye ukuta huku mawakala wakijaribu kulizuia japo hawakufanikiwa na kura zikapeperushwa na upepo.

Kufuatia hali hiyo uchaguzi katika ngazi ya mwenyekiti uliahirishwa na umerudiwa jana Jumanne huku mgombea wa CCM Bala Nundo akiibuka mshindi katika uchaguzi akimshinda mgombea wa Chadema.


Mtandao Huu Unakujali,Ni Wako!! Tunataka Tukutumie Habari zetu Zote Mara Tu Tunapozipandisha Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa Sasa Hivi ><<VITUKO>>,"MAPENZI",<<HABARI MSETO>>MAGAZETI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527