Joto ya Chadema Shinyanga !! VIONGOZI WA CCM WATAKA KUCHAPANA MAKONDE OFISINI ,KISA KUSHINDWA NA CHADEMA

Kushoto ni katibu wa CCM taifa ndugu Abdulrahman Kinana,katikati ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga ndugu Khamis Mgeja,kulia ni katibu wa siasa na uenezi CCM taifa ndugu Nape Nnauye wakiwa pamoja katika moja ya ziara yao mkoani Shinyanga ambapo kati ya mambo waliyoyazungumzia ilikuwa ni kusisitiza juu ya uadilifu wa viongozi wa chama-Picha kutoka Maktaba ya Malunde1 blog

Vurugu ya aina yake imetokea kwenye ofisi za Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini baada ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kushinda kwa kishindo katika kata ya Ngokolo hali iliyosababisha viongozi wa ngazi za juu wa  CCM kuanza kushikana uchawi kwamba nani kasababisha anguko hilo.

Malunde1 blog inaambiwa kuwa jana majira ya saa tano asubuhi katibu wa siasa na uenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Charles Shigino almanusura atwangane makonde na kuishia kutukanana matusi ya nguoni na katibu wa umoja wa Vijana wilaya ya Shinyanga Mjini (UVCCM), Zawadi Hussein.

Varangati hilo lilitokea wakati Shigino akiingia katika ofisi za chama hicho ambapo ghafla alitokea katibu wa umoja wa vijana (UVCCM Hussein na kumzuia kuingia katika ofisi hizo na kuanza kumrushia maneno machafu akimtuhumu kuchangia kufanya vibaya katika kata ya Ngokolo ambapo Chadema wamepata ushindi katika  mitaa 6 na CCM wakiambulia mtaa mmoja pekee.

“Wakati  naendelea kujitetea, aliendelea kuniporomoshea matusi mfululizo ,ndipo uzalendo ukanishinda na mimi nikaanza kujihami na kusababisha ugomvi mkubwa nje ya ofisi ya chama, na kujaza umati wa watu waliofika kushuhudia ugomvi huu, ambao hauna maana zaidi ya kukiaibisha chama”,Shigino aliiambia Malunde1 blog. 

Katibu wa umoja wa Vijana wilaya ya Shinyanga Mjini Zawadi Hussein amesema alimzuia Shigino kuingia katika ofisi za chama hicho kwa madai kuwa yeye ni msaliti wa chama na amekuwa akitoa siri za CCM na kuzipeleka kwa wapinzani.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja ameiambia Malunde1 blog kuwa CCM mkoa bado haijapata taarifa za wilaya kuhusu uchaguzi na kwamba watafanya kikao cha  tathmini kuhusu uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita na kujadili taarifa kutoka wilaya zote ili kujua changamoto na mafanikio yao ikiwa ni pamoja na sakata la mgogoro huo uliojitokeza baina ya viongozi hao wa chama hivyo kwa sasa hawezi kuzugumzia suala la viongozi hao.

Katika uchaguzi huo wilaya ya Shinyanga Mjini kati ya mitaa 55 CCM, wamepata mitaa 26, CHADEMA mitaa 29.

Kata iliyoleta kizaa zaa ni ile iliyokuwa inaongozwa na diwani Sebastian Peter Mzuka maarufu OBAMA ambaye alirubunika kisha kuhamia CCM ambako pia alivurugwa na kurudi Chadema akidai kuwa ndiyo chama chenye uleta ukombozi japokuwa mpaka sasa haajajibiwa na mamlaka zinazohusika juu ya hatma ya udiwani wao  baada ya kuandika barua kuomba kurudishiwa udiwani wake na mwenzake Zacharia Mfuko kutoka kata ya Masekelo ambako pia mitaa yote imezolewa na CHADEMA katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika juzi.

Na Kadama Malunde-Shinyanga

Mtandao Huu Unakujali,Ni Wako!! Tunataka Tukutumie Habari zetu Zote Mara Tu Tunapozipandisha Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa Sasa Hivi ><<VITUKO>>,"MAPENZI",<<HABARI MSETO>>MAGAZETI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527