MBUNGE MWANAMKE WA KENYA ASIMULIA ALIVYOVULIWA NGUO BUNGENI





Muheshimiwa Millie Odhiambo ni mbunge wa eneo bunge la Mbita nchini kenya aliyedaiwa kuwa wabunge wenzake walijaribu kumvua nguo wakati walipokuwa wakipinga mswada wa usalama uliopitishwa katika bunge hilo siku ya Alhamisi.

Kufuatia vurugu na purukushani zilizoonekana katika bunge la Kenya wakati wa kupitishwa kwa mswada wa usalama ,mbunge mmoja mwanamke sasa amejitokeza na kudai kwamba wabunge wenzake watatu wanaume walijaribu kumvua nguo.
Mbunge huyo Millie Odhiambo aliandika katika mtandao wake wa facebook kwamba wabunge wengi walipigwa huku yeye akidai kupigwa ngumi machoni na mbunge mmoja kabla ya wabunge wawili kujaribu kumvua nguo.
Hivi ndivyo ujumbe huo ulivyosoma katika mtandao wake wa facebook:
''Tulijaribu kulemaza kikao hicho asubuhi yote.lakini ilipofika mwendo wa saa nane waliwasili wakiwa wamejitayarisha ya kutosha.Wabunge wengi walipigwa.Mimi mwenyewe nilipigwa ngumi machoni na mbunge mmoja huku wengine wawili wakijaribu kunivua nguo.lakini mimi si wa kulia lia kwamba nimepigwa kofi! Mbunge aliyenipiga amejua kwamba mimi ni mbunge wa Mbita aliyechaguliwa na wala si kuteuliwa.Walipojaribu kunivua nguo mimi mwenyewe niliwamalizia kuwavulia nguo.Mimi siogopi na nashkuru nilivyoumbwa.Sitakubali kutishwa kwa kutumia jinsia yangu'',aliandika bi Millie..
Maandishi haya baadaye yalifuatiwa na mengine yaliosema kuwa ameenda kupigwa picha na kuangaliwa jicho lake hospitali.
via>>BBC
Mpenzi Msomaji,Tunapenda kukutumia Habari zetu zote mara tu Tunapoziweka Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post