BAADA YA MAXIMO KUTIMULIWA YANGA,VAN DER PRUIJM ATUA RASMI DAR

van pruijm

Kocha Van Der Pruijm akiwa na Shaffih Dauda mara tu baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere

Kocha wa zamani wa Yanga mdachi Hans Van Der Pruijm amesema amerudi tena kwenye timu yake ya zamani kuendeleza pale alipoishia,

‘Falsafa yangu ipo pale pale ya kucheza soka la kushambulia, kwasababu naamini ili ushinde mchezo ni lazima ufunge mabao ya kutosha’.

VAN PRUIJM 1
Van Der Pruijm akifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Clouds TV mara tu baada ya kutua  saa nane na nusu usiku wa kuamkia leo.

Kocha huyo amesema bado hajasaini mkataba ila ana matumaini makubwa atamalizana na wakurugenzi wa klabu pale watakapokutana,

Van Pruijm anakuja kuziba pengo la kocha aliyetimuliwa Mbrazil Marcio Maximo .


Mtandao Huu Unakujali,Ni Wako!! Tunataka Tukutumie Habari zetu Zote Mara Tu Tunapozipandisha Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa Sasa Hivi ><<VITUKO>>,"MAPENZI",<<HABARI MSETO>>MAGAZETI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527