Wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa
kujenga desturi ya kupima afya zao mara kwa mara ili kusaidia kutambua afya
zao ikiwa ni pamoja na kupata huduma na
ushauri juu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Kauli hiyo imetolewa leo katika kijiji cha Mwime Kata
ya Mwendakulima na mratibu wa Ukimwi wa halmashauri ya Mji wa Kahama Elibariki
Minja wakati akizungumza kwenye mashindano ya kutafuta kikundi bora cha
utunzi wa nyimbo zenye maudhui ya Ukimwi kuelekea siku ya Ukimwi Dunia Disemba
mosi.
Amesema kama wananchi watakuwa na mwamko wa
kupima afya zao, itasaidia jamii kutambua madhara
ya VVU, pamoja na kujua mbinu za kujilinda na kujikinga na maambvukizi mapya ya
Ukimwi na kwamba njia pekee ya kufikisaha elimu kwa wananchi ni
pamoja na viongozi na mashirika kuendelea kutoa elimu.
Minja amewataka wananchi kutambua
kwamba wilaya ya Kahama ndio inayoongoza kwa kwa kuwa na
idadi kubwa ya maambukizi ya Ukimwi katika mkoa wa Shinyanga,hivyo jamii haina
budi kutambua madhara pamoja na mbinu ya kujilinda.
Kwa upande wake Afisa mahusiano wa Mgodi huo Davidi
Kilala amesema lengo la kufanya mashindano hayo ni kupata kikundi
kitakachoelimisha jamii juu ya ukimwi, jinsi ya kujikinga na
maambukizi mapya ya ukimwi kwa pamoja na unyanyapaa njia ya Sanaa.
Amesema tayari wamekwisha kupata kikundi cha Tuaminiane ambacho
kitaungana na vikundi vingine kutoka Mwendakulima na
Chapulwa kupata mwakilishi wa kata hiyo atakayekwenda
kuhamasisha kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambapo
wilaya ya Kahama itafanyika katika kata ya Lunguya katika
halmashauri ya Msalala.
Kwa upande wake Kaimu Afisa mtendaji wa Kata
hiyo Marry Bukwimba amewataka wananchi wa kata
hivyo kuzingatia ushauri unaotolewa na viongozi wa serikali na Mgodi
wa Buzwagi ili kupata jamii yenye ulelewa wa kutambua
mabaya na mazuri.
Nao baadhi ya wananchi wametoa pongezi kwa
Mgodi wa Buzwagi, kwa kubuni hamasa ya vikundi katika vijiji ambapo
wameomba serikali na wadau wengine kujitokeza kuhamasisha ili jamii
itambue jinsi ya kujikinga na Maambukizi ya VVU.
Na Ndalike Sonda-Kahama