Utamaduni Lake Zone_SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU "GAMBOSHI" SEHEMU YA NANE


Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE",angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya NANE  ya simulizi ya kusisimua kuhusu Gamboshi



SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU GAMBOSHI SEHEMU YA 8

 MAZINGIRA; Shinyanga vijijini.
Simu yake-0765676242(WhatsApp)
 timotheomathias0@gmail.com

Maana ya maneno yaliyotumika kwenye simulizi

-GAMBOSHI ni makazi au eneo linalotumika kuhifadhia misukule.
-MSUKULE‬ ni mtu aliyechukuliwa kwa njia ya kishirikina (kichawi) akiwa mzima (hai), lakini kwa upeo wa kawaida ni dhahiri kuwa amekufa
Ilipoishia.......................
Baada ya kufikisha miaka 38 mama mlezi wangu alikufa na siku hiyo ndiyo alinisimulia haya yote na kunirithisha mambo ya uchawi na kuniambia niokoe watu kama mimi alivyoniokoa".

Kipindi anatusimulia nilishangaa kumuona babu amenyamaza kimya na kuanza kutetemeka mwili mzima na baadae kishindo kilisikika kutoka juu mpaka chini ya sehemu tuliyokuwa tumesimama na mkuu wa wachawi alisimama mbele yetu wakiwa wameangaliana na babu huku sisi macho yakitoka mithili ya chura aliyebanwa mlango.........

Endelea................
Mkuu wa wachawi alionekana kukasirika sana kwa jinsi muonekano wake ulivyokuwa.
Mkuu wa wachawi alimsogelea taratibu babu na kuanza kusema.....

"Nilikulazimisha sana kujiunga na mimi lakini ulikataa kumbe malengo yako ni haya ya kipuuzi, mpaka unafikia hatua ya kuniulia watu wangu!????"
Kipindi hicho babu anaulizwa maswali alikuwa kimya na kajasho kembamba kakimtiririka mwilini.

Wakati mkuu wa wachawi anamfokea babu, Babu alinikonyeza kwa ishara kwa kutumia kidole chake cha mkono wa kushoto.

Babu kulingana na ishara aliyokuwa anaitumia nilimwelewa sana kwani alinihitaji pete niliyokuwa nimevaa niivue, lakini sikuelewa niivue niiweke wapi?.

 Sheila naye aliniminya kwenye kidole cha mguu wa kushoto na kunikonyeza kuwa pete niiachie chini.

Kabla sijafanya chochote nilishikwa na butwaa kwa mambo aliyokuwa anayafanya mkuu wa wachawi, kwani juu ya bega la lake alitua bundi mkubwa sana ukimwangalia usoni mfano wa binadamu.

Baada ya muda kidogo ndege mwingine aina ya kasuku alitua juu ya bega la mkuu wa wachawi.

Taratibu wale ndege mmoja baada ya mwingine walianza kubadilika na kuwa binadamu.
Bundi alibadilika na kuwa binadamu wa kizungu mwanaume, mfano wa miaka 55 si mzee sana wala kijana.

Upande wa pili naye kasuku alibadilika na kuwa mtu mweupe wa kike naye si mzee sana. 

Kimoyomoyo nilijiuuliza kumbe na wazungu wachawi wapo?
Wote kwa pamoja wachawi walijipanga msitari mmoja na kushikana mikono, ikiwa wachawi wa kizungu wamevalia mavazi meupe.

Walianza kuomba dua zao ambazo mimi nilikuwa sielewi lugha walikuwa wanatumia.
Ghafla babu alianza kubadilika na mwili wake kuwa kuku mwenye manyoya meupe.

Kitendo cha babu kubadilishwa na kuku nakumbuka kuwa aliniambia nivue pete lakini nilisahau, harakaharaka pete nilianza kuiuvua kwa umakini ili kusudi wasinigundue kama navua pete mkononi.

Kweli niilifanikiwa kuivua na kuliachia chini na hakuna aliyeweza kugundua.

Baada ya kitendo cha kuivua pete na kuidondosha chini, Sheila alidondoka chini, puani zilianza kumtoka damu akiwa anapiga kelele na miguu yake akiirusha rusha kama mtu mwenye degedege.

Nikiwa nashangaa mkuki ulinichoma ubavuni mwangu na kutokezea upande wa pili, damu ilimiminika sana, baada ya dakika mbili fahamu ziliniishia na kudondoka chini nasikuweza tena kujua Kipi kiliendelea baada ya hapo.
*****************
Nilikuja kuzinduka nipo katikati nimezingirwa na watu wa kila aina wakiwemo wazungu, pia wote walivalia mavazi meupe na mimi nilivikwa mavazi meupe na kuwekewa ushungi tofauti na wao walivyo kuwa wamevalia kwani mavazi yao hayakuwa na ushungi.

Kimoyomoyo nilijiuliza mimi si nilikuwa nimechomwa mkuki???, nikajishika ubavuni sikuona alama au makovu ya aina yoyote! Au naota???
 Ina maana Sheila wangu ndiyo amekufa??? Maswali mengi sana nilijiuuliza lakini sikupata jibu. Taratibu machozi yalianza kunitiririka.

Mkuu wa wachawi aliinuka na kuja moja kwa moja sehemu nilipokuwa nimekaa, kabla hajasema chochote alinisujudia kwa kushika kifua chake na kuinama mbele yangu.

Alipomaliza kunifanyia hayo yote alianza kusema
 "kwanza kabisa bwanaTimothy nakupongeza kwa nafasi uliyoweza kupewa ya kwenda Nigeria kuwakilisha vijana wenzio katika kambi yetu. Katika nchi ya Tanzania mtaondoka vijana 6 kutoka kambi mbalimbali".

Vijana wengine watano waliletwa katikati tukawa vijana sita, na mbele yetu vikakeletwa nyungo sita. Mchawi mmoja alikuja akiwa amebeba visigino vya binadamu na kuanza kutugawia kila mmoja wetu alienea.
Kisigino kilikuwa kibichi kilionekana kimetoka kukatwa muda si mrefu kutoka kwa binadamu.

Mkuu wa wachawi alianza kutuelekeza na kutupa masharti alisema, kisigino ndiyo rimoti yenu, pia na matumizi yake alituelekeza.

Alitusisitiza kuwa tusipite karibu na kanisa la aina yoyote.
Kila mmoja wetu alikaa kwenye ungo wake tayari kwa safari ya kwenda Nigeria.....

Itaendelea wiki ijayo siku ya Jumamosi kupitia www.malunde1.blogspot.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527