ANGALIA PICHA_KINANA AANZA ZIARA YAKE MKOANI LINDI


1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivalishwa Skafu na vijana na wa Chipukizi wakati alipowasili eneo la Somanga wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi akianza ziara yake ya siku 16 katika mikoa ya Lindi na Mtwara akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza sughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi, Katibu Mkuu huyo anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi pamoja na Mjumbe wa NEC mkoa wa Lindi na Mbunge jimbo la Mtama Mh. Bernald Membe.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SOMANGA-KILWA)
3
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Wilaya  ya Kilwa na Mkoa wa Lindi waliofika katika eneo la Somanga kwa ajili ya mapokezi Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa.
4
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliofika kumpokea katika eneo la Somanga wilayani Kilwa kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi.
5
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Ndugu Abdallah Ulega wakati akielekea kushiriki ujenzi wa jengo la VICOBA  Mwamko Somanga.
6
Mmoja wa wasanii Ali Said Abubakary akicheza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
7
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa VICOBA Mwamko Somanga.
8
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua ukumbi wa VICOBA Mwamko Somanga.
10
Mjumbe wa NEC mkoa wa Lindi na Mbunge jimbo la Mtama Mh. Bernald Membe akizungumza na wananchi katika mji wa Somanga mara baada ya kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
11
Mkuu wa mkoa wa Lindi Magalula Sid Magalula akiwasalimia wananchi huku Katibu Mkuu wa CCM akinyanyua mkono wake juu kuashiria kupokea salamu zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post