Utamaduni Lake Zone_SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU "GAMBOSHI" SEHEMU YA 7




Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE",angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya SABA  ya simulizi ya kusisimua kuhusu Gamboshi


SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU GAMBOSHI SEHEMU YA 7

 MAZINGIRA; Shinyanga vijijini.
Simu yake-0765676242(WhatsApp)
 timotheomathias0@gmail.com

Maana ya maneno yaliyotumika kwenye simulizi

-GAMBOSHI ni makazi au eneo linalotumika kuhifadhia misukule.
-MSUKULE‬ ni mtu aliyechukuliwa kwa njia ya kishirikina (kichawi) akiwa mzima (hai), lakini kwa upeo wa kawaida ni dhahiri kuwa amekufa
Ilipoishia.......................

Tukiwa tunamimina dawa nilishangaa kumuona bibi akianguka chini na kupiga kelele kama mtoto mdogo.
 Hapo ndipo nilishuhudia wanafunzi wakipiga kelele na kushangilia huku wanatoka madarasani na kuelekea ofisini na wengine wakimzingira bibi.
Baada ya muda mfupi wanakijiji walijaa shuleni na kumuamuru bibi avue nguo, kweli alivua nguo zote na alibakia kama alivyozaliwa...
Endelea....................

Bibi alitembezwa kijiji kizima akiwa uchi huku mwili wake ukiwa umepakwa tope na kubebeshwa mzigo wa kuni kichwani.
Aliweza kutolewa nje kidogo ya kijiji (porini), niliweza kumshuhudia bibi akifa huku akiwa uchi wa mnyama.

Kabla ya kifo chake alifungwa kitambaa usoni na kufungwa kamba shingoni iliyounganishwa moja kwa moja kutoka juu mti.
Kamba hiyo ilivutwa kwa nguvu na watu watatu toka chini.

Nilimshuhudia bibi akipiga kelele kama mtoto mdogo, taratibu kinyesi kilianza kuchuruzika huku mkojo ukimtoka.
Baada ya dakika mbili bibi alikata kauli/alifariki.
Taratiibu!!!! Niligeuza macho yangu upande alipokuwa amesisima Sheila na kumkuta machozi yakimtoka.
Nilishindwa kujizuia hisia zangu, machozi yalinilenga machoni na kujikuta tukikumbatiana na Sheila, (kipindi hicho kwa macho ya kibinadamu ya kawaida tulikuwa hatuonekani).
Wanakijiji wote walisambaa kutoka katika eneo la tukio, lakini nilibaki mimi na Sheila tukiwa tumekumbatiana na pembeni kukiwa na mzoga wa bibi yetu.
Nilijikaza kiume na kuanza kuikata kamba iliyotumika kumyonga marehemu bibi.
Kabla sijaanza kufanya chochote, Sheila aliniita kwa sauti ya juu sana akiwa mkono wake anasonta nyuma yangu.

 Niligeuka na kushuhudia joka kubwa sana likija kwa kasi huku likinifuata nilipokuwa nimesimama.

Nilianza kukimbia nikiwa namfuata Sheila kama kufa tukafe wote mbele ya safari. 

Kulingana na sipidi niliyokuwa nayo hatimaye niliweza kumpata Sheila.
Kitendo cha kumpata tu! Mbele yetu alitokea nyoka mwingine mfano wa yule tunayemkimbia, ilitubidi tusimame tu!, maana hakuna ujanja na siku za mwizi ni arobaini na leo ni siku yetu ya kufa.
Joka ambalo lilikuwa linatukimbiza lilipotukaribia lilisimama pia na joka la mbele lilifanya vivyo hivyo.

 Tulibaki tumeduwaa huku hatuna hili wala lile, ghafla nyuma yangu niliguswa na kitu cha baridi sana.
Niligeuka haraka haraka na kumkuta akiwa ni babu ambaye huwa ananisaidia siku zote nikiwa katika kipindi kigumu.
Babu alianza kucheka sana huku akisema kumbe ni waoga kiasi hicho?? Poleni sana kwa kuwasumbua ila ni mojawapo ya mazoezi.

 Nilimjibu asante, lakini moyoni nilikasirika sana kwa kitendo alichonifanyia.
Babu nilimuuliza kwa nini unatufanyia hivyo?
Babu alisema nafanya hivyo kwa sababu ya maisha yenu kuyaokoa.

Nilimuuliza kivipi?
Babu alijibu, nilishangaa sana ulipochukua maamuzi ya kumkatia kamba huyo bibi! Wakati mimi nina mpango niwamalize wachawi wote wadogo wadogo nibaki na mkuu ambaye ni moto wa kuotea mbali upande wangu.
Kweli babu alikuwa akinisaidia kwa mambo mengi sana, lakini sikuweza kumjua jina lake na kwa nini alichukua maamuzi ya kunisaidia?,
Babu nilimuuliza jina lako unaitwa nani? Na kwa nini umechukua maamuzi ya kunisaidia?
Babu alitabasamu na kunijibu,

"Kwa jina naitwa babu mkombozi, kulingana ninavyookoa watu kutoka utumwani na kurudi uraiani.
Nimeamua kukusaidia maana maisha niliyoishi ni zaidi unayoishi wewe na mwenzio.
Kwa mujibu ya bibi wawili walionilea ni kwamba:

Siku ya kuzaliwa kwangu hosipitalini ndiyo ilikuwa siku ya oparesheni ya wachawi kwenda kuchukua watoto wachanga katika hospitali hiyo.
Na mimi ni miongoni ya watoto walioweza kuchuliwa kutoka katika hospital hiyo.
Siku ya kuchemshwa kuwa mafuta, sufuria lilijaa na mimi ikanibidi nisubilie awamu inayokuja.

Na nafasi hiyo bibi alinichukua na kwenda kunihifadhi kwake alinilea kama mtoto wake akisaidiwa na rafiki yake na wote kwa pamoja niliwaita mama.
Nilipofikisha miaka 17 rafiki yake bibi alifariki na kubakia mmoja, na kipindi hicho chote masuala ya uchawi alikuwa akinifundisha na mpaka mkuu alinitaka sana katika kazi zake za kichawi lakini mama alinizuia sana.
Baada ya kufikisha miaka 38 mama mlezi wangu alikufa na siku hiyo ndiyo alinisimulia haya yote na kunirithisha mambo ya uchawi na kuniambia niokoe watu kama mimi alivyoniokoa".
Kipindi anatusimulia nilishangaa kumuona babu amenyamaza kimya na kuanza kutetemeka mwili mzima na baadae kishindo kilisikika kutoka juu mpaka chini ya sehemu tuliyokuwa tumesimama na mkuu wa wachawi alisimama mbele yetu wakiwa wameangaliana na babu huku sisi macho yakitoka mithili ya chura aliyebanwa mlango.........

Itaendelea wiki ijayo siku ya Jumamosi kupitia www.malunde1.blogspot.com


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527