HAYA HAPA MAJINA YA ABIRIA WALIOFARIKI NA MAJERUHI KATIKA AJALI YA HIACE LEO SHINYANGA
Tuesday, November 25, 2014
Hiace yenye namba za usajili T761 CKD ikiwa imepinduka baada kuparamia tuta la barabarani na kupoteza mwelekeo kisha kutumbukia mtaroni katika eneo la Buhangija mjini Shinyanga barabara ya Tinde-Shinyanga leo saa nne na nusu asubuhi-Picha na Kadama Malunde
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limesema waliofariki dunia katika ajali ya Hiace yenye namba za usajili T761 CKD iliyotokea le asubuhi mjini Shinyanga ni 9,majeruhi 9.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SSP Longinus Tibishubwamu amewataja waliofariki dunia kuwa ni Nkingwa Kariagi(50) mkazi wa Mwamanota Kishapu,Kelvin Michael(21) utingo wa gari hilo,mkazi wa Ngokolo,mjini Shinyanga na Masanilo Jisandu(miaka 50) mkazi wa Negezi Kalitu Kishapu. Wengine waliofariki dunia ni Amina Abdallah,mkazi wa Mbika Kahama,Nkola Shija(20) mkazi wa Kahama,Elizabeth Ngusa (15) mkazi wa Maswa na wengine watatu hawajajulikana majina,umri,kabila wala makazi yao.
Majeruhi katika ajali hiyo ni 9,ambao ni
Peter Yustasi(49) mkazi wa Sengerema,Frola Ngudungi(35) mkazi wa Ushetu Kahama,Yesaya Samwel(40) mkazi wa Singida,Kwimba Damayake(36) mkazi wa Iramba Tabora na Nyanzobe Henge(70) mkazi wa Uloa Kahama. Majeruhi wengine ni Katumbi Nangi(36) mkazi wa Uloa Kahama,Emmanuel John(22) mkazi wa Mwakitolyo,Jimoda Kaliagi(52) mkazi wa Mwamanota Kishapu na Kalwa Mwandu(36) mkazi wa Kahama.
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin