![]() |
| Wakazi wa Kahama wakiwa eneo la ajali leo asubuhi |
Watu wanne wamefariki dunia wilayani Kahama mkoani Shinyanga baada ya basi walilokuwa wanasafiria kupinduka katika kona ya Phantom barabara ya kutoka Kahama kwenda Isaka mkoani Shinyanga baada ya dereva wake kushindwa kulihimili kutokana na kile kilichodaiwa kuendesha katika mwendokasi.
Tukio hilo limetokea leo saa 12 asubuhi katika
eneo la Phantom kilomita chache kutoka kituo kikuu cha Mabasi mjini Kahama baada ya basi aina ya Scania lenye namba za usajili T
412 CGN mali ya Wibonela Ambalo lilikuwa likitokea mjini Kahama kwenda jijini
Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka.
Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi kuendesha mwendokasi wakati akitoka katika
kituo kikuu cha mabasi mjini Kahama na alipofika kwenye kona ya kutoka mjini
Kahama kuelekea Isaka.
Mashuhuda waliiambia malunde1 blog kuwa dereva alikuwa anashindana na mabasi mengine mengine kuelekea eneo la mizani kupima uzito mjini Kahama.
Wamesema kufuatia mwendokasi huo basi kona ilimshinda huku yeye akiruka kutoka kwenye gari na kuangukia katika mtaro na basi kupinduka mara tatu huku yeye akitorokea kusikojulikana.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kahama walikolazwa majeruhi 40 Dkt Joseph Ngowi amesema watu waliopoteza maisha wanne ambao ni Amina Emmanuel ambaye alikuwa mjamzito mkazi wa Kigoma, Salum (amefahamika kwa jina moja) mtoto wa miezi mitatu Robin Jordan na mwanamme mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja.

Dkt Ngowi amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa
ni Maulid Shaban (44) mkazi wa Ushirombo, Athuman Issa (21) mkazi wa Kahama,
Jordan Mbeya (28) mkazi wa Kasulu, Brandina Patrick (24) mkazi wa Kasulu, Oscar
Lameck (19) Mkazi wa Kigoma, Stamili Shaban (38) mkazi wa Dodoma, Neema Dastan
(18) Mkazi wa Kahama na Monica Gadson (35) mkazi wa Kahama.
Majeruhi
wengine ni Nickson Andati ambaye ni Mchungaji mkazi wa nchi ya Rwanda (34)
Lucas Mlezi (48), Joyce Fred (28) Asnath Remtula (27) , Eveline Hamis (6),
Happy Hamis (30), Japhet Masha (29), Jackson Elisanto (26), Buligelila Ramadhani
(40) na Rita Bryson (25) wote wakazi wa Kahama.
Pia
kuna Irene Wilson (17) mkazi wa Kasulu, John Lembo(45) Mkazi wa Bariadi, Hamis
Shaban (31) mkazi wa Kahama, Emmanuel Lambambo (32) mkazi wa Kigoma, Kashindye
Masanja (28), Frenk Kishimba (21) Peter Bahati (22) wote wakazi wa Kahama,
Iseme Hilila (36) mkazi wa Katoro Geita, Ebrania Saga (30) mkazi wa Kigoma, na
Anika Amdani (35) Mkazi wa Kahama.
Wengine
ni Shaban Omary (16) ambaye ni mkazi wa Dodoma,Grolia Moses (18) mkazi wa
Kahama, Agnes Broto (35) Mkazi wa Ngara, Kulwa Said (40) mkazi wa Kahama, Peter
David (42) mkazi wa Kahama,Tunga Lazaro (22) mkazi wa Bariadi, na Happy David
(32) huku majeruhi wengine wakishindwakutambulika kutokana na kuwa mahututi.
Miili ya marehemu ipo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa ajili ya kutambuliwa na ndugu wa marehemu na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu huku wanne wakiripotiwa kuwa hali zao ni mbaya.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha aliyekuwa eneo la tukio na kutembelea majeruhi hospitalini amesema majeruhi ni 40 na kwamba jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi juu ya ajali hiyo huku likimtafuta dereva wa basi hilo Godfrey Prochas aliyekimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Malunde1 blog inawapa pole ndugu jamaa na marafiki waliofikwa na msiba.
Mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu.Amina.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
Wakati huo huo mwanamme ambaye jina lake halikuweza
kujulikana mara moja ameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi waliojichukulia
sheria mkononi baada kumtuhumu kuiba mali za abiria waliopata ajali katika basi
hilo eneo la tukio.
Mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu.Amina.
Na Kadama Malunde-Shinyanga

Social Plugin