MZUKA WAPANDA,MSANII ADONDOKA JUKWAANI NA KUUMIA KICHWA AKITOA BURUDANI KWA MASHABIKI

Busta Rhymes Ajeruhiwa Katika Show

Mwanahiphop Mkongwe Busta Rhymes amejeruhiwa vibaya na kuvuja damu katika maeneo ya Kichwani baada ya kuanguka alipokua akiwapa mashabiki wake mikono katika show moja ya mjini New York.
Nyota huyo aliyewahi kutamba na wimbo wa ' I know What You want' akishirikiana na Mariah Carey alihudhuria Show hiyo na akatumbuiza jukwaani ndipo akiwa na furaha kueleke a kwa mashabiki wake aliamua kufika ukingoni mwa jukwaa hilo na kuamua kushikana mikono na mashabiki hao kama ishara ya upendo kwao ndipo alipoanguka katika jukwaa hilo refu na kuumia kichwani
Wanausalama walifanikiwa kumtoa katika eneo ambalo alianguka na kuonekana akiwa anatokwa na damu nyingi kichwani
Hata hivyo muda mfupi baadae Busta aliwatoa wasiwasi mashabiki wake na kuwashukuru kwa upendo wao mkubwa na kukiri kua alikua amepatwa na maumiv katika baadhi ya sehemu za mwili wake kupitia mtandao wa twitter 

BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527