MWINGINE AVULIWA NGUO HADHARANI HUKO KENYA_ 100 WAKAMATWA KUHUSIKA,WENGI NI WALEVI




Bofya Maneno haya Tukutumie Habari zetu moja kwa moja kwako kila siku
Wanawake mjini Nairobi waliandamana kupinga kisa cha kumvua nguo mwanamke kwa kuvalia nguo fupi

Polisi mjini Nairobi wamewakamata watu 100 katika msako baada ya mwanamke mwingine kuvuliwa nguo katika mtaa wa mabanda wa Kayole mjini Nairobi.
Inadaiwa mwanamke huyo alikuwa amevalia nguo zisizo za heshima.
Naibu kamanda wa polisi mjini Nairobi Moses Ombati, amenukuliwa akisema wengi wa waliokamatwa walikuwa wanaume walevi.
Bwana Ombati aliongeza kusema kwamba, mwanamke huyo alishambuliwa katika mtaa wa Kayole Jumatatu jioni na kwamba polisi wanaendelea na msako.
Mnamo Jumatatu mamia ya wanawake waliandamana katika barabara za katikati mwa mji kulaani kitendo cha kumvua nguo mwanamke mwingine mapema mwezi huu mjini Nairobi.
Wanawake hao waliandamana kufuatia wito kwenye mitandao ya kijamii chini ya kauli mbiu #MyDressMyChoice yaani vazi langu uamuzi wangu au nitavaa nitakachojiamulia mwenyewe.
Waandamanaji hao wakiwemo wanawake mashuhuri, wanasiasa na wanaharakati waliandamana hadi katika kituo cha mabasi ambako mwanamke wa kwanza alidaiwa kuvuliwa mavazi yake kwa madai alikuwa amevalia 'Mini Skirt'
via>>bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post