Jingine Jipya!! JESHI LA POLISI LATANGAZA NAFASI ZA KAZI,SHARTI UWE NA "BIKIRA",VIDOLE VYATUMIKA KUBAINI KAMA UNA BIKIRA AU LA!!


Serikali ya Indonesia inaelezwa kuruhusu kuwafanyia wanawake wanaotaka kujiunga na Jeshi la Polisi kipimo cha bikira ,shirika la Human rights Watch limeeleza.
Shirika hilo uangalizi wa haki za binaadam liliwahoji Polisi wanawake na wanaotaka kujiunga na Jeshi la polisi ambao tayari wamepimwa katika miji sita ya nchini Indonesia,wawili kati yao wamefanyiwa kipimo hicho mwaka huu.

Kipimo cha bikira kimeorodheshwa kuwa moja ya matakwa ya kuingia kwenye Jeshi, tovuti ya polisi imeeleza.
Wanawake waliofanyiwa kipimo hicho wamesema walipata maumivu na kujisikia kudhalilishwa.
Askari wa kike walishapeleka malalamiko kwa ngazi za juu za jeshi la Polisi bila mafanikio.
Afisa wa juu wa Human Rights Watch,Nisha Varia amesema kipimo hicho ni unyanyasaji na kinawadhalilisha wanawake, amewataka polisi mjini Jakarta kufuta kipimo hicho na kukipiga marufuku nchi nzima.
Polisi nao wanasema kuwa hawafanyi kipimo hicho kwa sasa kwa kuwa wamepiga marufuku.

Hata hivyo hakuna ushahidi wa kutosha kuwa Jeshi la Polisi limesitisha kitendo hicho kwa kuwa katika tovuti yake eneo la kazi tangazo la tarehe 5 mwezi Novemba mwaka 2014 imeeleza kuwa wanawake wanaotaka kuwa polisi wanapaswa kujaribiwa kama wana bikira,hivyo basi wanawake wanaotaka kuwa askari wanapaswa kutunza bikira zao.
Wanawake walioolewa hawapewi nafasi hiyo.
Mashuhuda wanasema kuwa jaribio la bikira hufanywa katika hospitali zinazoendeshwa na jeshi la Polisi, vidole hutumika katika kubaini kama mwanamke ni bikira au la.
Shirika la Human Rights Watch limesema kipimo hiki hufanywa na Polisi pia nchini Misri, India na Afghanistan.
via>>Kibonajoro.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post