Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SHINYANGA ASHUHUDIA MECHI AKIWA AMEKAA KWENYE GOGO KUBWAAAA!!


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja  akiwa amekaa kwenye gogo akiwa katika uwanja wa kijiji cha Isaka kata ya Isaka akiwa na watoto akiangalia mechi ya kirafiki kati ya timu ya Isaka Star na Home Boys zote kutoka jimbo la Msalala linaloongozwa na mbunge Ezekiel Maige wilayani Kahama mkoani Shinyanga-Picha na Kadama Malunde


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja  akikagua timu hizo kabla ya kuanza mchezo huo(jezi nyesi ni timu ya Home Boys).Mgeja alisema ili kuinua sekta ya michezo nchini ni vyema halmashauri za wilaya mkoani Shinyanga zikawa mstari wa mbele kusaidia sekta ya michezo kwa kutenga fedha kwa ajili ya michezo huku akisisitiza umuhimu wa kukarabati na kujenga viwanja-Picha na Kadama Malunde

Mchezo kati ya Home Boys(jesi nyeusi) na timu ya Isaka Star(jezi ya njano) ukiendelea,inagwa hadi mwisho wa mchezo Isaka star bao 1,Home Boys -0.Mshindi akaondoka  na zawadi ya mipira miwili -Picha na Kadama Malunde

Baada ya mchezo kuisha wachezaji wa Isaka Star wakisubiri zawadi yao-Picha na Kadama Malunde
 Mchezaji wa Isaka Star akipokea zawadi ya mipira miwili kutoka kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja-Picha na Kadama Malunde
Baada ya kupewa zawadi vijana wananyanyuka kurudi majumbani mwao jana jioni/usiku -Picha na Kadama Malunde
Usiku uliingia wengine wakasema hawaondoki uwanjani hadi wapige picha na mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja-Picha na Kadama Malunde

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com