ULIIPATA YA WAUMINI WA KANISA LA ANGLIKANA HUKO MWANZA KUDAI KUWA ASKOFU WAO NI MFUASI WA FREEMASONS? BASI ITAZAME HAPA

 
Waumini wa kanisa la Anglikana Wilaya ya Nyamagana Mwanza walisimamisha kwa muda shughuli za ibada kanisani hapo baada ya kutokea vurugu kubwa.

 Vurugu hizo zilitokea baada ya baadhi ya waumini hao kumtuhumu Askofu wa kanisa hilo Boniface Kwangu kwamba ni mmoja wa wafuasi wa kundi la Freemasons na hufanya kazi za kundi hilo.

Mmoja wa waumini wa kanisa hilo Shadrack Lazaro alitoa 
tamko la jinsi askofu wao anavyofanya kazi na kundi la Freemason ndipo waumini walipomvamia na kumtoa nje ya kanisa kwa nguvu na kusababisha vurugu kubwa.

Muumini huyo alisema pamoja na sababu kadhaa za kumkataa askofu huyo pia hawaridhishwi na tabia yake ikiwemo kutaka kubomoa sakafu akidai kuna Hirizi imefichwa na baadhi ya  waumini wake kanisani hapo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post