Kweli Mjini Shule!! JAMAA ATAPELI KWA KUJIDAI MGONJWA MAHUTUTI KWA MUDA WA MIAKA 2,KUKWEPA VYOMBO VYA DOLA

  • 23 Oktoba 2014
Alan Knighty alijidai kuwa mgonjwa mahututi ingawa alikamatwa na madaktari akiwa anajilisha
Mwanamume mmoja alitumia udanganyifu na kujidai kuwa mgonjwa mahututi kwa miaka miwili nchini Uingereza.
Alan Knight, mwenye umri wa miaka 47, kutoka mtaa wa Swansea, alimuibia mzee mmoja jirani yake pauni elfu arobaini kwa njia ya udanganyifu na kudai kuwa hengeweza kutembea kutokana na kupooza kutoka shingoni hadi miguuni.
Hii ilikuwa njama yake ili asiweze kukamatwa kwa kosa hilo.
 Inaarifiwa alikwepa polisi mara mbili kwani wakati yupo yeye mwenyewe alijipeleka hospitani ili asikamatwe na kushitakiwa.
Knight na mkewe madukani
Kila wakati polisi walipotaka kumfikisha mahakamani , Knight alijipeleka hositalini akidai kuwa hali yake imekuwa mbaya zaidi.
Hata hivyo siku zake za mwizi kushikwa zilifika pale wauguzi walipompata katika chumba chake hospitalini akiwa anakula , kupanguza mdomo wake na hata kuandika.
Kwa miaka miwili, Night alikwepa mkono wa sheria kwa kudai kuwa alikuwa hawezi kuamka wala kutembea na pia alikuwa tayari na uraibu wa kutumia gesi ya oxygen kama mtu ambaye hawezi kupumua bila usaidizi wa gesi hiyo.
Yote hayo yalikuwa ongo na ambayo yangewezekana tu kwa sinema.
Hapa Knight alinaswa kwa kamera ya CCTV na polisi akiwa madukani
Alan Knight katika duka la Tesco, alinaswa na polisi kwa camera ya CCTV akisukuma gari la kubebea bidhaa ndani ya duka hilo wakati akidai kuwa mgonjwa mahututi.
Afisa mmoja wa polisi Paul Harry,kutoka South Wales alisema:
 ‘Katika kazi yangu hii, sijawahi kuona kisa kama hicho ambacho kilipangwa na kutekelezwa kwa umakini huo.''
Mkewe Knight ndiye alikuwa msaidizi wake katika sakata hii akimhudumia wakati wote
Mkewe mwanamume huyo mwenye watoto watatu , pia alikuwemo kwenye sakata kwani siku zote alionekana akimhudumia mumewe aliyejidai kuwa hali mahututi. 
Mbunge wa eneo la Swansea West aliambia BBC kuwa: "Nilikutana na Bi Hellen na akaniarufu ambavyo mumewe alikuwa na hali mbaya ya kiafya na kwamba walitendewa vibaya na polisi.''
Knight anakabiliwa na mashitaka 19 ikwemo wizi na ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527