TANESCO SHINYANGA KICHEFU CHEFU,UMEME UNAKATWA UNARUDISHWA-WANANCHI WAVUNJA UKIMYA

Ni siku ya kama ya tatu leo mjini Shinyanga kumezuka kitendo cha Shirika la umeme nchini kukata kukata umeme kila dakika hali ambayo imeleta hofu kwa wateja wa shirika hilo kuunguziwa nyumba na vitu vyao.


Wakizungumza na malunde1  blog wakazi wa Shinyanga wameeleza kukerwa na tabia ya TANESCO kukata umeme ovyo kila dakika na kurudisha tena bila hata kutoa taarifa ya kwanini wanakata na kurudisha.

Hata hivyo Kaimu Meneja Tanesco mkoa wa Shinyanga Arthur Gama amesema kata kata hiyo ya umeme inatokana na pale mafundi wanapokuwa wanafanya marekebisho ya hitilafu, na kujaribu kama tatizo hilo limetengemaa na hivyo wanazima wanawasha.


Amesema kuna tatizo limetokea katika line ya kusafirisha umeme maeneo ya viwanda, mtaa wa Matanda mjini Shinyanga tangu juzi na wanaendelea na matengenezo

HISIA ZA WANANCHI KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
+++++++++


TANESCO shinyanga hivi mmeanza kucheza kamali na wananchi? Huo umeme wenu wakamali toka juzi ni nin? kama mko kwenye ufundi kwanini msizime jumla au mtoe tangazo tujue maan mimi siwasomi kabisa huu umeme ndani ya lisaa moja unakatika mara4 jamani ni komborela kuwa mnatutambia mmejitokeza au mmejificha tuwatafute? Acheni basi utani na mali za watu nini maan ya TANESCO TUNAKUANGAZIA MAISHA YAKO au ni kinyume TUNAKUUNGUZIA MAISHA YAKO? binafsi nimechukia mno cjui wew mwana shy mwwnzangu
UnlikeUnlike ·  · 


++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Tanesco mniache kidogo basi nimalize kazi yangu asee ndo muendelee na hilo zoezi la zima washa zima washa nimechoka sana pls.
LikeLike ·  · 

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++


Tanesco si bora mkate umeme moja kwa moja siyo kukata kata hovyo,utaratibu gani huo dakika 5 mnakata,mara sekunde 40 mnarudisha..NI shinyanga tu au na mikoa mingine!?
LikeLike ·  · 


+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Hivi TANESCO mna nini? mnatukatia umeme tena mnakata kila baada ya dkk 10 tunashindwa kuwaelewa mna tatizo gani? mnajuwa mnakera ni bora mtutangazie tatizo mlilonalo tujue kuliko mnavotufanyia.au mnataka mtuunguzie vitu vyetu? ah! mnaboa bana kila siku nyinyi tu.lini tutaenjoy na TANESCO?
LikeLike ·  · 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post