HUYU NDIYO MSHINDI /MISS LAKE ZONE 2014,ANATOKA MKOANI GEITA,NAMBA 2 NA 3 KUTOKA SHINYANGA

 Mkurugenzi wa Lenny Hotel Leonard Bugomola akikabidhi funguo za gari kwa Miss Lake zone 2014 Rahel Clevery-Picha na Valence Robert-Malunde1 blog

Mshindi wa kwanza/Miss Lake Zone 2014-Rahel Clevery akiwa ameshikilia funguo za gari la milioni 10 alilopewa kama zawadi ya ushindi-Picha na Valence Robert-Malunde1 blog

Hatimaye kitendawili cha nani atakuwa Miss Lake Zone Mwaka 2014 kwa warembo kumi na nane (18) kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa kimeteguliwa baada ya Rahel Clevery kutoka Geita kuibuka mshindi na kuondoka na  gari lenye thamani ya Tsh. Milioni Kumi lililotolewa na mkurugenzi wa Lenny Hotel  iliyoko mkoani Geita- Leonard Bugomola.

Mashindano hayo yamefanyika juzi katika uwanja CCM Kirumba jijini Mwanza na kuhudhuriwa na watu wachache ambapo mgeni  rasmi alikuwa  Leonard Bugomola ambaye ni mkurugenzi wa Lenny Hotel.

Akiwahutubia wananchi hao wachache pamoja na warembo hao aliwataka washiriki wa shindano hilo kuendelea kutunza nidhamu kama walivyoishi kwake kwa kipindi chote hicho hata watakapokwenda kwenye mikoa yao waendelee kuwa hivyo kwa kuwaheshimu wote.

Bugomola alishangazwa na kitendo cha  watu wa mkoa wa Mwanza  kuwa wachache katika viwanja hivyo  japokuwa walitangaziwa siku nyingi.

"Jamani mimi, Mgeni rasmi sikutegemea kama watu wa Mwanza watakuwa wachache kiasi hiki  ,maana Geita walifurika sana na huku mmetangaziwa kwa kipindi kirefu sana kuhusu shindano hili",aliongeza

Hata  alisema yeye ataendelea kudhamini mashindano mengine na kuomba kibali kupitia kwa Ashim Lundenga kama itawezekana shindano la Miss Tanzania mwaka ujao lifanyike mkoani Geita.

Akipokea zawadi ya Gari hiyo Miss Lake zone 2014 Rahel alisema kuwa atahakikisha anatangaza vivutio vyote vilivyoko katika mkoa wake na kutoa shukrani zake kubwa kwa Mkurugenzi wa Lenny Hotel ambaye amekuwa ni msaada mkubwa kwao kwa kipindi chote cha siku kumi walichokaa kambini kwa kujifunza  nidhamu na heshima kwa watu wote.

Mshindi alioweza kuibuka kidedea katika mashindano hayo ni Rahel Clevery kutoka Geita, aliyenyakua gari lenye thamani ya Tshs. Mil. 10 lililotolewa Mkurugenzi wa Lenny Hotel iliyoko Mkoani Geita.

Mshindi wa pili ni Mary Emmanuel  kutoka Shinyanga na mshindi wa tatu ni Nicole  Sarakikya kutoka Shinyanga na  mshindi wa nne ni Dorini Robert kutoka Mwanza.

Na Valence Robert-Malunde1 blog-Mwanza

ANGALIA PICHA ZA GARI NA WAREMBO WOTE HAPA

TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post