Hatari!! JAMBAZI ALIYEVUNJA DUKA NA KUIBA,AUAWA KWA KIPIGO CHA WANANCHI,POLISI WALIMSHTUKIA

Jambazi mmoja akiwa na bunduki na risasi 47 pamoja na sare za jeshi la wananchi ameuawa na wananchi weye hasira kali wakati akijaribu kukimbia baada ya kufanya tukio la kuvunja duka na kuiba shilingi laki 7 katika eneo la melela Mvomero mkoani Morogoro.

Kamanda Polisi mkoa wa Morogoro Lenard Paul amemtaja mtuhumiwa amefahamika kwa majina ya Antony Msandawe mkazi Kilosa Maghubike jambazi hilo usiku lilifanya tukio la kuvunja duka ambapo alikua njiani kulekea kilosa kufanya tukio jingine.

Hata hivyo  askari wa barabarani walimstukia ndipo wananchi wakasaidiana na jeshi la polisi kumkimbiza ambapo alikamatwa na kupigwa na wananchi na alifariki dunia akiwa njiani kueleka  hospitali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527