Wizi wa watoto Geita_MTOTO HUYU KAIBIWA ,LEO SIKU YA 10,HAJULIKANI ALIPO

Mtoto Emmanuel Jeremiah, miezi 9 mkazi wa kata ya  Rwamgasa - Mkoani Geita ambaye hadi sasa hajulikani alipo 
 Mtoto Emmanuel Jeremiah, miezi 9 mkazi wa kata ya  Rwamgasa - Mkoani Geita
 Helena Asunga mkazi wa Mgusu - Geita anayedaiwa kumuiba mtoto Emmanuel

IKIWA ni siku chache  tu baada ya malunde1 blog  kuripoti kushamiri kwa vitendo vya kuibiwa kwa watoto wadogo katika Mkoa wa Geita na kupelekwa kusikojulikana tukio jingine limetokea tarehe saba mwezi huu majira ya saa nane mchana ambapo mtoto Emmanuael Jeremiah miezi (9) mkazi wa Mgusu  kuibiwa na kutokomezwa kusiko julikana mpaka sasa.
 
Akizungumzia juu ya tukio hilo juzi baba mzazi wa mtoto huyo Jeremia Emmanuel  alisema siku hiyo jirani yake aliyejulikana kwa jina la Helena, Asunga miaka(32) mjaluo  alimkuta  akiwa nje ya Nyumba yao na  kumchukua mtoto na kutokomea naye kusiko julikana mpaka sasa.
 
Jeremia aliongeza kuwa  yeye na mke wake Lilian Jeremia walikuwa ndani ya nyumba na walipotoka nje walikuta mtoto wao hayupo na kuambiwa na jirani yake kwamba kachukuliwa na Helena na hawakuanza kumtafuta kwani ilikuwa ni kawaida jirani huyo huwa anamchukua na kumrudisha.
 
Alisema ilipofika saa kumi jioni siku hiyo alikwenda kwa jirani huyo na kuuliza kama Helena yupo na kukuta hayupo na alipouliza mtoto wake aliambiwa hajafikishwa pale na kuanza kumsaka kila kona lakini jitihada za kumpata ziligonga mwamba na kwenda kuripoti katika kituo cha polisi Mgusu na kupewa RB BKR/IR/68/2014.
 
Matukio ya kuiba watoto katika mkoa wa Geita yanazidi kushamiri huku wanaoiba huwapoteza watoto hao na kuwataka wazazi wao kutoa kiasi kikubwa cha fedha ili warudishe au huwaelekeza walipo mara baada ya kutoa.
 
Jeshi la polisi mkoani hapa limethibitisha kutokea kwa tukio na uchunguzi wa kubaini chanzo cha kuibiwa kwa mtoto huyo unaendelea na mtuhumiwa bado anatafutwa.

Na Valence Robert-Malunde1 blog-Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post