WATANZANIA WATAKIWA KUTHAMINI WAWEKEZAJI WAZAWA

Watanzania wameshauriwa kutoa vipaumbele kwa wawekezaji wazalendo na kuondoa vikwazo dhidi yao ili kuongeza nafasi za ajira hususani kwa vijana wanaoishi katika maeneo hayo kuliko kuachia fursa hizo kuwa urahisi kwa wawekezaji kutoka nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa juzi na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi  kata ya  Busanda  wilayani geita  mkoani Geita bwana  Renatus Pandajilima kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya kata hiyo kwa lengo la kujadili mgogoro uliopo kati ya baadhi ya wananchi na mmoja wa muwekezaji mzawa  wa kata hiyo  Elias Kisomi.

Alisema kuwa wazawa wanatakiwa wapewe kipaumbele zaidi ili kuongeza nafasi ya ajira ambayo ni changamoto kubwa ya sasa kwa taifa na kuondoa vikwazo dhidi yao hali ambapo inawakatisha tamaa na kuwafanya kushindwa kuwekeza katika nchi yao na kuamua kuondoka kwenda kuwekeza katika nchi nyingine.

Baadhi ya wananchi katika kata hiyo ya Busanda wameanzisha mgogoro na muwekezaji huyo kwa madai ya kuwa mwekezajihuyo amewadhurumu ardhi yao kwa kutofuata taratibu za umiliki huku wakisababisha mwekezaji huyo kushindwa kuanza shughuli za uchenjuaji wa dhahabu katika eneo alilopewa.

Aidha baadhi wa wajumbe wa serikali ya kijiji pamoja  na wananchi wameshangazwa na kusikitishwa na kitendo hicho na kukiita cha kihuni kwani walishakaa katika mikutano ya hadhara mbalimbali na kuhalalisha eneo hilo kuwa ni la Elias Kisomi baaada  ya yeye kuomba kulimiki eneo hilo.

Mwananchi mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe alisema.......

 “Mimi nashangaa na ninajiuliza watu wanaodai eneo hili ni lao wametoka wapi,wakati mikutano ya kijiji kuanzia mwaka 2012  tulikubaliana wote kwa pamoja na majina pamoja na sahihi zetu na tulimpa eneo hili bwana Kisomi ,hawa watu yawezekana wametumwa na kuna mchezo mchafu unaendelea".

Naye mtendaji wa kata hiyo  Justina  Mabala  alipoulizwa kuhusu mmiliki halali wa eneo hilo ni nani ,alisema mgogoro huo aliukuta na mahakama ya ardhi ya wilaya ilikwisha kutoa hukumu ya uhalali wa mmiliki wa eneo hilo na kushangazwa na watu wanaojitokeza na kusababisha migogoro hali ambayo inazorotesha shughuli za maendeleo katika kata yake.

Mara baada ya mkutano huo Malunde1 blog  ili lazimika kumtafuta mwekezaji huyo mzalendo Elias Kisomi,ambapo alieleza kusikitishwa na na  mambo anayofanyiwa.

Alisema anakatishwa tamaa kwani tangu alipo kabidhiwa eneo na kwamba yeye ndiye alibuni wazo hilo ili kuweka fursa ya vijana kupata ajira katika kata yake kuliko kukaa vijiweni.

Na Valence Robert-Malunde1 blog-Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post