STAND UNITED YAENDELEA KUJINOA,YAITANDIKA HEKIMA FC YA MWANZA 3-1


Katika kuendelea na ziara yake ya kukipima kikosi chake kujiandaa na ligi kuu Soka Tanzania bara timu ya stand utd ya mkoani shinyanga leo imeshuka dimbani kucheza na Hekima fc ya jijini Mwanza katika uwanja wa shule ya msingi Ibanda ulioko Mkolani.

Mpaka dakika tisini za mchezo zinakamilika stand utd 3-1 Hekima fc.

Alikuwa ni Judy Filimon aliyenza kuwasabahi Stand utd ktk dakika ya 15 ya mchezo,dakika 29 ya mchezo Mussa Kimbu akaisawazishia Stand utd kwa kichwa.

Zikiwa zimesalia dakika 10 kwenda mapumziko Kamana Salum akaiandikia Stand utd bao la Pili.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinakamilika Stand utd 2 Hekima fc 1. 

Kipindi cha Pili kilianza kwa kasi huku Hekima fc wakitafuta nafasi ya kusawazisha lakini ngome imara ya Stand utd iliyokuwa ikiongozwa na Jisendi Mathias iliondosha hatari zote langoni.

Kalamu ya magoli ya Stand utd ilihitimishwa na Kharidi Seleman katika dakika ya 74 ya mchezo na mpaka dakika 90 za mchezo zinakamilika Stand utd 3 Hekima fc 1.

Na Isaack Edward-Mwanza

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post