JAMAA "MCHAWI" AKATALIWA KUINGIA DUBAI,KISA ANA MAPEMBE NA KATOGA MWILI MZIMA


Picha: Mwenye vipuli usoni na tattoo nyingi zaidi duniani azuiwa kuingia Dubai

Mwanamume wa Ujerumani ambaye anaongoza rikodi ya dunia kuwa na mwili uliotogwa mara nyingi kabisa amekataliwa ruhusa ya kuingia Dubai, baada ya kwenda huko kutokeza katika klabu ya starehe.
Rolf Buchholz, ametogwa mwahala 453 kwenye mwili na uso wake na ana pembe mbili kwenye kipaji.
Ameeleza kwenye mitandao ya kijamii kuwa alikataliwa na maafisa wa uwanja wa ndege kuingia nchini kwa sababu, kama alivosema, alikuwa "mchawi".

Bwana Buchholz ameapa kuwa hatarudi tena Falme za Kiarabu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post