Hii kali!! MREMBO AMEZA SIMU ILI BOYFRIEND WAKE ASISOME SMS ZA MAHABA ZA NJEMBA NYINGINE

Screen Shot 2014-08-01 at 8.33.09 AM
Kuna zile habari ambazo hata ziwe zimetokea miezi au miaka mingapi nyumba, huwezi tu kuzisahau kwa sababu sio za kawaida kuzisikia au kuzishuhudia kabisa.

Tumekua tukisikia visa vingi sana vinavyotokana na mapenzi, yaani pale Mwanamke au Mwanaume anakuta msg za ajabu baada ya kuchukua simu ya mpenzi wake ila hii ya Brazil imevunja rekodi.

Imetokea kwa binti mmoja kumeza simu muda mfupi tu baada ya boyfriend (Renato) wake kutaka kusoma msg ambapo msichana alikimbia na simu kutoka kwenye mikono ya boyfriend na kuimeza kwa kuhofia angeikamata simu.

Ilibidi akimbizwe hospitali na kufanikiwa kutolewa hiyo simu tumboni ambapo haikujulikana ni nini ambacho mrembo huyu alikua anakificha kwa boyfriend wake ila iliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani kwamba tayari mrembo huyu alikua na mwanaume mwingine nje ya uhusiano.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post