DAKTARI MWINGINE WA EBOLA AFARIKI DUNIA

Ripoti kutoka Sierra Leone zinasema kuwa daktari mwengine amefariki kutokana na virusi vya ugonjwa wa Ebola.
Afisa huyo aliambukizwa ugonjwa huo wakati alipokuwa akiwatibu wagonjwa wa Ebola.
Zaidi ya maafisa 20 wa afya wameaga dunia katika taifa hilo huku wengine wengi wakifanya mgomo wakidai marupurupu yao.
Awali ,liberia ili-ufungua mtaa mmoja wa mabanda uliokuwa umetengwa kwa kipindi cha juma moja ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.
Zaidi ya watu 1500 wamepoteza maisha yao magharibi mwa Afrika kutokana na kuzuka kwa ugonjwa huo hatari mnamo mwezi Machi.
via>>BBC

TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527