ANGALIA PICHA AJALI YA FUSO NA DALADALA ILIYOUA WATU 10 NA KUJERUHI 7 HUKO MBEYA

9
Hivi ndivyo ambavyo Daladala hiyo ilivyojibamiza muda mchache uliopita
Eneo hili la ubavuni ndipo eneo ambalo Daladala hiyo iliingia na Kujigonga
Gari hilo aina ya Tata likiwa limepaki pembeni Muda mchache baada ya kupata ajali hiyo.
3
Askari wa usalama wa Barabarani akiwa anatazama na kuchunguza zaidi ajali hiyo.
Eneo ambalo Daladala hiyo iliyofumuka
Viti vikiwa vimeharibika baada ya ajali kutokea.
Hivi ndivyo Daladala hiyo iliyokuwa ikitoka Mwanjelwa kuja Mbalizi ilivyo  Haribika Baada ya ajali hiyo.
Mashuhuda wakiwa wamelizunguka daladala hiyo kushuhudia kllichotokea.
 Hapa ndipo eneo ambapo ajali imetokea , Askari wa usalama wa barabarani wakiendelea kufuatilia ajali hiyo
 Ilikuwa ni ajali mbaya.
Mashuhuda.

WATU kumi wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili.
Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari ndogo ya abiria maarufu daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota Hiace  na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 CSV.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso ilikuwa ikiingia barabarani.
Walisema inasemekana dereva wa Hiace gari yake ilimshinda kutokana na kutelemka mlima mkali wa Mbalizi inagawa pia walimtupia lawama dereva wa Fuso ambaye alikuwa akiingia barabarani bila kuchukua tahadhari.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali teule ya Ifisi Mbalizi, Sikitu Mbilinyi, ambako Majeruhi na marehemu walikimbizwa hapo alithibitisha kupokea majeruhi 7 ambapo alisema kati yao ni wanawake 3 na wanaume 4.
Alisema kati ya majeruhi hao wawili wamepewa rufaa kwenda hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kuhitaji msaada zaidi huklu wengine wakiendelea kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru hali zao.
Mbilinyi aliongeza kuwa pia wamepokea miili ya marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na Wanawake wanne na Wanaume wanne.
Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu hayajaweza kupatikana mara moja kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo Dereva wa Fuso akitokomea mara baada ya tukio.
via>>Mbeya yetu blog

TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527