SHUHUDA HAPA TUKIO ZIMA LA MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA LEO MKOANI SHINYANGA


Hapa ni katika mnara wa kumbukumbu ya mashujaa uliopo katika eneo la Mazingira senta mjini Shinyanga.Mnara huo ulijengwa mwaka 1972.Pichani ni wananchi na viongozi wa mkoa wa wakiwa kwenye  mnara huo mapema leo wakati wa maadhimisho ya siku ya mashuja

Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga ndugu  Anna rose Nyamubi akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa katika maadhimisho ya siku ya mashujaa ambayo yamefanyika mazingira senta ,mahali  palipojengwa mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.
Mhasibu mkuu wa serikali mkoa wa Shinyanga Burton Mwakanyamale akiweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa leo
Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akiweka upinde na mkuki katika mnara huo ishara ya  kuwakumbuka mashujaa waliopigana vita ya pili ya dunia
Afisa uhamiaji mkoa wa Shinyanga ndugu Anna maria Yondani akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Shinyanga leo .
 Mzee Omari Mbushi mkazi wa kijiji cha Bugayambelele manispaa ya Shinyanga, ambaye alipigana vita ya pili ya dunia akiweka shoka kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.
Viongozi wa madhehebu ya dini na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakiwa eneo la mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.
Wananchi wakiwa katika eneo la mnara wa mashujaa
Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annarose Nyamubi ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ,akiweka ngao kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa katika viwanja vya mazingira senta mjini Shinyanga.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga,kulia ni kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha
Viongozi wa serikali wakiwa eneo ulipojengwa mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.Picha zote kwa hisani ya Stella blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post