AJALI YA FUSO KISHAPU_6 KATI YA MAJERUHI 46 WAPELEKWA BUGANDO,MAJINA YAKO HAPA

lori lenye namba za usajili T680 ARL aina ya Fuso lililokuwa limepakiza mizigo na wafanyabiashara ambao idadi yao bado haijajulikana  likitokea kijiji cha Kiloleli wilayani Kishapu kwenda katika mnada wa Mhunze uliopo Kishapu,likiwa katika eneo la tukio katika kijiji cha Usunga kilometa chache kufika eneo la mnada wa Mhunze
Wananchi wakiangalia fuso  ambalo jana liliacha njia na kupinduka katika kijiji cha Uchunga wilaya ya kishapu mkoani Shinyanga na kuuwa watu watatu huku 46 wakiwa ni majeruhi wakati likielekea kwenye mnada wa Mhunze ambapo wengi waliokuwa ndani ya gari hilo ni wafanyabiashara.    
                                                             

Majeruhi 6 kati ya 35 waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga baada ya kupata ajali wakati wakisafiri na gari aina ya fuso,lililopinduka jana asubuhi katika eneo la Uchunga wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga wamepelekwa katika hospitali ya rufaa jijini Mwanza kwa ajili ya matibabu zaidi.

Majeruhi wengine 11 jana walikimbizwa katika hospitali ya Kolandoto.

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Daniel Maguja amewataja waliopelekwa  Bugando  kuwa ni  Masanja Kishiwa 42 mkazi wa Mwajiginya),Mayala Lugomela (31 mkazi wa Jijongo,Malando Mashamindi(20) mkazi wa Nobola,Marco Bundala 19 mkazi wa Jijongo, Jeremia Jisena 35 mkazi wa Mwaweja na Ndila Shigela 41 kutoka kijiji cha Mwajiginya wilayani Kishapu. 

Amewataja waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo kuwa ni ni Charles Makengwa,  Difa Shimo miaka 28 wote wakazi wa wilaya ya Kishapu na kwamba maiti moja ndugu zake bado hawajapatikana ili kuitambua. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post