Aliyesimama ni mkurugenzi wa VETA kanda ya Magharibi Hildegardis Bitegera Bana akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya UMIVUSTA kanda ya magharibi ambapo alisema michezo hiyo ilianzishwa mwaka 1996 hapa nchini lakini kanda ya magharibi mwaka 2007 ikiwa na lengo la kuwakutanisha vijana wanaosoma katika vyuo vya ufundi mbalimbali nchini ili waweze kuonesha viapaji vyao katika michezo ikiaminika kuwa kwa kupitia michezo hiyo vijana hao wangeweza kubadilishana uzoefu na kujenga urafiki na ushirikiano miongoni mwao,kujenga afya bora ya akili na mwili ili kumudu vyema masomo yao kiufundi.
Aliyesimama ni mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mashindano ya UMIVUSTA kanda ya magharibi ambaye alikuwa afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga ndugu Charles Maugira ambapo aliwaka vijana hao kutumia fursa waliyopewa ikizingatiwa kuwa sera ya taifa la Tanzania kwa sasa ni kukuza michezo kwenye taasisi za elimu ili kupata vijana wenye nidhamu na nguvu.Aliongeza kuwa michezo hujenga furaha na ushirikiano na kichocheo muhimu katika kujifunza na kwamba sasa hivi michezo ni ajira yenye ujira bora zaidi.
Wadau wa michezo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi
Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga ndugu Charles Maugira akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya UMIVUSTA ambapo michezo ya aina nne imeanza kufanyika leo katika viwanja vya Veta mjini Shinyanga.Michezo hiyo itafanyika kwa siku kumi kuanzia leo na michezo itakayofanyika ni mpira wa miguu,pete,mpira wa wavu na riadha kwa mbio fupi.
Wadau wa michezo wakiwa katika viwanja vya Veta Shinyanga leo jioni
Mgeni rasmi Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga ndugu Charles Maugira (mwenye kofia mbele) akikagua timu ya mpira wa miguu ya VETA Shinyanga(wenye jezi za njano),nyuma yake ni mkurugenzi wa VETA kanda ya Magharibi Hildegardis Bitegera Bana akifuatiwa na mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga bwana Afridon Mkhomoi ambaye ndiyo mwenyeji wa mashindano ya UMIVUSTA kanda ya magharibi mwaka 2014
Mwenye suti ni mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga ndugu Afridon Mkhomoi akishikana mikono na wachezaji wa timu ya Veta Tabora pamoja na waamuzi wa mchezo uliokuwa unafuata,aliyeshikilia kitabu ni Mratibu wa UMIVUSTA kanda ya magharibi Rodrick George
Timu kati ya veta Shinyanga(kulia) na timu ya Veta Tabora (kushoto) zikiwa uwanjani kabla ya mechi kuanza ikiwa ni mechi ya pili kwa siku ya leo ya kwanza ilikuwa kati ya timu ya mpira ya Veta Nzega vs Tabora Network ambapo mshindi alikuwa Veta Nzega walioibuka na ushindi wa bao 2-1
Timu ya Veta Tabora ikiwa uwanjani kabla ya mchuano wake na timu ya veta Shinyanga
Timu ya mpira wa miguu ya veta Shinyanga ikiwa uwanjani kabla ya mechi
Mechi kati ya Veta Shinyanga na Veta Tabora ikiwa inaendelea ambapo hadi mwisho wa mchezo Veta 0 huku Veta Tabora-1
Tunaangalia mechi...........
Mchezo unaendeleaa
Tunashangiliaaaa
Tunashuhudia mechi....
Michezo ya UMIVUSTA ilifanyika moja kwa moja katika ngazi ya taifa hadi mwaka 1997 ambapo michezo iliamuliwa ichezwe kwenye ngazi ya kanda na baadaye ndiyo iendelee kwenye ngazi ya taifa,na kanda ya magharibi imenza kufanyika mwaka 2007 na mwaka huu 2014 ni mara ya 3 ya kufanyika.
Katika kufanikisha mashindano hay Vyuo shiriki vimechangia gharama za usafiri na chakula kwa wanavyuo wao ambapo ofisi ya veta kanda ya magharibi imegharamia ununuzi wa sare za michezo kwa ajili ya ufunguzi,gharama za waamuzi wa michezo yote,pia imenunua mipira yote,zawadi kwa washindi,masurufu ya mratibu,gharama za maji,umeme na kuni n.k
Gharama za huduma ya kwanza zimendaliwa na ofisi ya mkurugenzi wa kanda ambapo jumla kuu ya gharama zilizotumika na zitakazoendelea kutumika hadi mwisho wa mashindano hayo ya umivusta ni shilingi 8,292,500/=
PICHA ZOTE NA KADAMA MALUNDE-MALUNDE1 BLOG- SHINYANGA
Social Plugin