TAZAMA PICHA-HOTELI YA KISASA YAFUNGULIWA MJINI SHINYANGA,NI "MAKINDO COMMERCIAL HOTEL" IPO MAJENGO KARIBU NA BAKURUTU

Hili ni jengo la Hoteli mpya tena ya kisasa inayojulikana kwa jina la “MAKINDO COMMERCIAL HOTEL” iliyopo katika eneo la Majengo mjini Shinyanga.Ipo nyuma ya Vijana Senta karibu na Bakurutu mjini Shinyanga.Hoteli hii ya kisasa imezinduliwa jana Jumapili Juni 8,2014 mgeni rasmi akiwa ni Mchungaji Daniel Maduhu kutoka kanisa la Waadventista wasabato manispaa ya Tabora na kuhudhuriwa na wakazi wa ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga.

Makindo Hotel ina vyumba 9,vyote vikiwa vifaa vya kisasa,Tv flat screen,Air Condition,simu ,friji,kabati,dressing table na bei za vyumba ni shilingi elfu 20 na kuna vyumba vya shilingi elfu 30 tu na kuna sehemu ya kupaki magari



Wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Hoteli ya Makindo ambayo umejengwa na wawekezaji kutoka mkoa wa Shinyanga ambao ni Familia ya Mze MAKINDO(wanayantuzu) ujenzi wa hoteli hii ya kisasa umekamilika ndani ya miezi 7.
Maranatha kwaya kutoka kanisa la Waadventista wasabato Lubaga mjini Shinyanga wakiimba wimbo wakati wa uzinduzi wa Makindo Commercial Hotel jana jioni ndani ya hoteli hiyo ambapo mamia ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga na nje ya mkoa walishuhudia tukio hilo muhimu.Katika wimbo wao waliwaomba watu wa kada mbalimbali akiwemo Rais Jakaya Kikwete kufika katika hoteli hiyo ya kisasa kwa vile hoteli hiyo ina sifa zote na usalama upo wa kutosha


Uzinduzi wa Makindo Commercial Hotel mjini Shinyanga Unaendelea


Kushoto ni mkurugenzi wa Makindo Commercial Hotel bwana Deus Kija Makindo mkazi wa mjini Shinyanga na muumini wa kanisa la wasabato Lubaga akiwasalimia wageni mbalimbali waliofika katika uzinduzi wa hoteli yao ya kisasa kabisa katika mkoa wa Shinyanga.Kulia kwake ni mshereheshaji mwinjilisti wa watu wote ambaye pia ni mkurugenzi wa Amazing Grace Supermarket mjini Shinyanga ndugu Jackson Sadick Mbula


Kushoto ni mkurugenzi  msaidizi wa Makindo Commercial Hotel bwana Nehemia Makindo ambaye pia ni kutoka familia ya Mzee Makindo ambao wameamua kuwekeza katika mradi wa hoteli na kuwa mfano wa kuigwa kwa wananchi wazawa wa nchi ya Tanzania kuthubutu kuwekeza badala ya kutegemea wageni kutoka nchi za nje


Waimba mashairi wakifanya yao wakati wa uzinduzi wa Makindo Commercial Hotel jana mjini Shinyanga


Pasta Simeo Soloma Makunja kutoka kanisa la Wasabato jijini Mwanza aliyekuwa amaembatana na mgeni rasmi akitoa neno fupi wakati wa uzinduzi wa hoteli ya Makindo ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka watanzania kubadilika na kuanza kuwekeza kama ilivyofanya familia ya mzee Makindo ya mjini Shinyanga.Aidha alitumia fursa hiyo kuwatahadhalisha wafanyabiashara wanaotumia nguvu za giza kuendesha shughuli zao kwani mali zinazotokana na ushirikina maara nyingi hazidumu hivyo kuwataka kumtegemea mungu zaidi katika kazi zao.Aliwataka wafanyakazi kuepuka ushirikina katika maeneo ya kazi na waajiri kutoa mishahara kwa wafanyakazi wao kwa wakati.


Meneja mkuu wa Makindo Commercial Hotel Ndugu Mathias Malack(mwenye shati jeupe) akikabidhi risala kwa mgeni rasmi Mchungaji Daniel Maduhu kutoka kanisa la Waadventista wasabato manispaa ya Tabora muda mchache baada ya kumaliza kuisoma


Mgeni rasmi Mchungaji Daniel Maduhu kutoka kanisa la Waadventista wasabato manispaa ya Tabora  akiwahutubia wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa Makindo Commercial Hotel ambapo aliwataka wakazi wa Shinyanga kuungana na kuwekeza katika miradi mbalimbali.Pia alitumia fursa hiyo kuwaasa wafanyabiashara na jamii kwa ujumla kuachana na imani za kishirikina zinazopelekea wakati mwingine mauaji ya albino,watoto,mke na hata mme kwa kuamini kwamba watapata utajiri


Waliosimama ni familia ya Makindo wa mjini Shinyanga walioamua kuungana kuanzisha mradi wa hoteli ya kisasa mjini Shinyanga ambayo ujenzi wake umechukua muda mfupi sana (miezi 7)


Katika uzinduzi wa hoteli hiyo mgeni rasmi Mchungaji Daniel Maduhu kutoka kanisa la Waadventista wasabato jijini Mwanza aliweka wakfu jengo hilo la hoteli,kukata utepe na kutembelea vyumba vya jengo hilo sambamba na kula chakula pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa hoteli hiyo ya kisasa mjini Shinyanga


Mgeni rasmi Mchungaji Daniel Maduhu kutoka kanisa la Waadventista wasabato manispaa ya Tabora  akikata utepe kuashiriria uzinduzi rasmi wa Makindo Commercial Hotel


Mgeni rasmi Mchungaji Daniel Maduhu kutoka kanisa la Waadventista wasabato manispaa ya Tabora (wa pili kutoka kushoto) akiwa ndani ya moja ya vyumba katika hoteli ya Makindo kushoto kwake ni ni mkurugenzi wa Makindo Commercial Hotel bwana Samwel Makindo


Moja ya chumba katika Makindo Commercial Hotel,pichani ni kitanda 


Kushoto ni mzee wa kanisa la Wasabato Lubaga mjini Shinyanga,akifuatiwa na mratibu wa sherehe za uzinduzi wa hoteli hiyo Daniel Mahenga pamoja wageni waalikwa akiwemo mgeni rasmi wakiwa ndani ya moja ya vyumba katika Makindo Commercial hotel


Mkurugenzi wa malunde1 Blog ndugu Kadama Malunde akapata fursa ya angalau kukaa kwenye kitanda katika moja ya vyumba vya Makindo Commercial Hotel ambapo ndani ya chumba hicho kuna vifaa vya kisasa pia kuna maji ya moto bila kusahau breakfast mida ya asubuhi unapoamka ambayo hutolewa bure kwa wateja wake


Wageni wote waliofika katika sherehe ya uzinduzi wa hoteli ya Makindo walipata fursa ya kula chakula


Wananchi wakiwa kwenye foleni kuelekea kwenye meza ya chakula cha Makindo Commercial Hotel

Picha zote na Kadama Malunde wa Malunde1 Blog Shinyanga




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post