MSICHANA ALIYEUA MAMA YAKE MZAZI KWA KUMCHOMA VISU MARA 151 AKWEPA JELA

Msichana aliyemuua mama yake kwa kumchoma visu mara 151 akwepa jela


Taarifa kutoka Colorado, Marekani zinaeleza kuwa Msichana mwenye umri wa miaka 19, anafahamika kwa jina la Isabella Yun-Mi Guzman ambaye alimchoma mama yake visu mara 151 ameachiwa huru.
Mahakama imemuachia huru Isabella baada ya kubaini kuwa ni mgonjwa wa akili na kwamba wakati anatekeleza tukio hilo hakuwa katika hali ya kawaida kiakili hivyo kwa mujibu wa sheria hana hatia.
Mahakama imeamuru msichana huyo kupelekwa katika hospitali ya wagonjwa wenye matatizo ya akili kwa ajili ya kupata matibabu badala ya kumpeleka jela.
Kwa mujibu wa ripoti zilizofikishwa mahakamani hapo na polisi, Issabella alimchoma mama yake visu mara 151 (Mara 35 usoni, mara 51 shingoni, na mara 65 katika sehemu nyingine za mwili.
Msichana huyo amepelekwa  Colorado Mental Health Institute. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527