KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI AWASHAMBULIA KAFULILA NA ZITTO,ASISITIZA KAFULILA NI TUMBILI TU

Photo: Katibu Mkuuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi awavaa Zitto na Kafulila!

- Adai ni washenzi na wala rushwa
- Asema nyaraka za IPTL wanazosambaza ni 'karatasi za kufungia vitumbua'
- Asisitiza Kafulila ni tumbili tu

VIDEO, habari kwa kina; soma => http://bit.ly/TDNmaJ
SAKATA linalohusu kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), limechukua sura mpya baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kuwashambulia kwa maneno makali, wabunge wawili Zitto Kabwe wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) na David Kafulila wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi).
FikraPevu ilikuwapo wakati Maswi akitumia maneno makali kwa kuyarudia, akikejeli nyaraka zinazotajwa kuwa ni ushahidi wa jinsi IPTL ilivyouza hisa zake na fedha kutolewa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika akaunti maalumu ya pamoja (Escrow), akisema nyaraka hizo ni karatasi za kufungia vitumbua zinazosambazwa na wabunge hao aliowaita “washenzi”.
Kauli hiyo ya Maswi imekuja siku mbili tu baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema kushambuliana na Kafulila kwa maneno makali malumbano yao yakianzia ndani ya Bunge na kuendelea walipotoka, kila mmoja akiamini kauli aliyoitoa ilikuwa ni sahihi.
Werema alimfananisha Kafulila na tumbili na yeye kumuita mwanasheria huyo mwizi. Tumbili ni mnyama wa porini wakati mwizi ni mtu anayetenda uhalifu kwa kuchukua kitu au mali isiyo yako.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI



chanzo-fikrapevu.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527