Inatishaaa!! GARI LAUA WAWILI NA KUJERUHI 36 WAKITOKA KUCHIMBA KABURI LA BIBI KIZEE,WANANCHI WAGOMA KUZIKA,MMOJA WA WAFIWA ATEMBEZEWA KICHAPO

Wananchi wa mtaa wa Uwanja kijiji cha Nyankumbu  katika kata ya Kalangala wilayani Geita mkoani  Geita wamegoma kushiriki mazishi ya kikongwe  aliyefariki katika ajali ya gari wakati wakitoka kuchimba kaburi.
Tukio hilo limetokea jana baada ya wananchi hao waliokuwa  wakitoka kuchimba kaburi  wakati  wanarudi ,wakiwa njiani ghafla gari aina ya fuso yenye namba za usajili T130 ACG waliyokuwa wamepanda ilichomoka tairi la   mbele la kushoto na kusababisha ajali ambayo  watu wawili  walikufa hapo hapo na wengine 36 kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita.
Akizungumza na Malunde1 blog kuhusu tukio hilo mwenyekiti wa maafa wa mtaa huo Mother Kazimoto alimtaja  aliyefariki  dunia katika msiba wa kwanza kuwa ni  Mariamu Kwangu(60) aliyefariki  tarehe 18 mwezi huu.

Pia aliwataja  watu wawili  waliofariki dunia siku ya pili baada ya fuso kuchomoka tairi kuwa ni Methew Benedicto(35) na Siwema Benima.
Katika haki iliyoacha watu midomo wazi Mama mzazi wa marehemu Methew ambaye ni Veridiana Lushinge baada ya kupata taarifa za kifo cha mtoto wake alienda kwa mke wa marehemu ambaye ni Sabina Maduka na kuanza kumpiga kwa kisingizio cha kuwa yeye amemuua mtoto wake jambo ambalo lilitafasiriwa na wananchi kuwa huenda imani za kishirikina zimetawala na kuamua kukataa kufanya mazishi kwa sababu za kumdhalilisha mama huyo mfiwa.
Hata hivyo wananchi hao walimuita mama huyo ili wamuulize kwa nini amempiga mfiwa lakini mama huyo hakuweza kuitikia wito huo jambo lililosababisha wananchi kushikwa na hasira za kutaka kufuata anakoishi kwani ni sehemu nyingine anapoishi na kwenye msiba.

 Hata hivyo kabla ya kufanya hilo mwenyekiti wa maafa wa mtaa wa Uwanja aliamua kutuliza tafrani hiyo baada ya wanandugu kuomba samahani kwa niaba ya mama yao huku wakiamriwa kutoa faini ya shilingi elfu thelathini.
Naye mama Sabina Maduka aliyefiwa na mme wake na kupigwa na mama mkwe wake alisema kuwa amesikitishwa na kitendo cha mama mkwe wake kumpiga wakati tukio la kifo cha mme wake kilisababishwa na ajali ya gari walipokuwa wanatoka kuchimba kaburi.

 "Nashangaa mama mkwe wangu kuja nyumbai kwangu na kuanza kunipiga na wakati anapewa taarifa za kifo hakuja hata kwenye msiba  wa mume wangu Methew Benedicto",alieleza Sabina.
Baadhi ya wananchi waolikuwa kwenye msiba walisema kuwa katika mtaa huo kumekuwa na matukio ya kutisha mwaka juzi familia moja watu 2 walikufa kwa siku moja na mwaka jana watu 2 walikufa kwa wakati mmoja na sasa bibi huyo(Mariamu Kwangu(60) ) amekufa yeye na watu 2 wamekufa na zaidi ya watu 33 wamejeruhiwa na kulazwa hospitali.

Na Valence Robert-Malunde1 blog-Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post