HUYU NDIYE MSHINDI WA TUZO YA BET

Hii ilikuwa siku nyingine muhimu kwa Tanzania na Africa kwa ujumla ambapo yalikuwa yanasubiriwa matokeo ya tuzo ya BET sana sana kipengele wanachowania tuzo wasanii wa Afrika akiwemo Diamond Platnumz. 

Davido kutoka Nigeria ndio amethibitisha kuwa mshindi wa tuzo hii ambapo kupitia page yake ya Instagram amewashukuru mashabiki na kuelezea furaha yake. 

Tuzo hii ilikuwa inawaniwa na Diamond Platnumz kutoka Tanzania, Mafikizolo wa South Africa, Sarkodie wa Ghana, Tiwa Savage wa Nigeria na Toofan wa Togo. 

Pamoja na kwamba Diamond hajawa mshindi wa tuzo hii, Watanzania wengi wamekua upande wake toka alipochaguliwa kuwania tuzo hizi na kumwambia hata kama hatoshinda, kuchaguliwa tu kushiriki BET ni zawadi ya kipekee na hatua kubwa kimuziki. 

Namkariri Rais Jakaya Kikwete pia aliesema ‘Hata kama asiposhinda Diamond, yenyewe kuchaguliwa kwenye tuzo za BET ni hatua kubwa kimuziki’ 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527