Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ALIYEPOTEA KATIKA MAZINGIRA TATANISHI AKUTWA AMEFUKIWA ARDHINI


Jeshi la polisi Mkoa  wa  Katavi  linawasaka watu watatu kwa tuhuma za kumuuwa na kisha kumfukia aridhini   Mbaya  Lukondia (36) mkazi wa Kijiji cha Kabunde  Kata ya Mamba  Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi .

Kamanda wa  jeshi la polisi wa Mkoa wakazi aliwataja watuhumiwa hao wanaotafutwa  kuwa ni  Ubakila  Kidakira , Jimon Dogi (lala)na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Omary  wote wakazi wa Kijiji cha Kabunde  Kata ya Mamba Wilaya ya Mlele .

Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari   ni  kwamba kabla ya kifo hicho marehemu  alitoweka nyumbani kwake  mwezi Aprili mwaka huu  na  haikuweza kueleweka mahali alipo kuwa .

Alisema kwa kipindi chote hicho ndugu wa marehemu  waliendelea kumtafuta  hadi hapo  june 19 alipogundulika  akiwa amefukiwa aridhini  huku mwili wake  ukiwa umeharibika vibaya .

Alifafanua  baada ya kufukuliwa kwa mwili huo wa marehemu na kufanyiwa uchunguzi ndipo ilipoonyesha kuwa marehemu aliuwawa kwa kupingwa na kitu kizito katika sehemu ya kichwani  na ubavuni.

Alisema watuhumiwa hao  wanadai  baada ya kufanya mauwaji hayo walitoweka  kijijini  hapo na mpaka sasa hawaja fahamika mahali walipo  kimbilia .

Alieleza  wananchi wa kijiji hicho waliwatila mashaka  ya  kuhusika na tukio hilo  baada ya mwili wa marehemu   kupatika  ukiwa umefukiwa aridhini na wao  toka siku huyo walitoweka  Kijijini .

Kamanda Kidavashari amesema jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi linaendelea kuwatafuta watuhuiwa hao watatu iliwakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Na  Walter Mguluchuma -Mpanda Katavi 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com