TAZAMA HAPA NJIA YA KUPAMBANA NA NDEGE KWENYE MASHAMBA YA MTAMA HUKO KISHAPU


Mkulima katika kijiji cha Mwamala kata ya Mwamashele katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga akitumia kombeo maarufu kwa jina la Nh’ago kwa kabila la Kisukuma kufukuza ndege aina ya Kwelea kwelea.


Hii njia mojawapo ya kupambana na ndege aina ya kwelea kwelea ambao wanashambulia zao la mtama kwa kasi ya ajabu katika kijiji cha Mwamala kata ya Mwamashele katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

Hii ni njia nyingine ya kupambana na ndege hao,ambapo wakulima wamefunga nguo kwenye mashamba ili kuwatisha ndege hao wasiingie katika mashamba yao
Pamoja na kujitahidi kulima zao la mtama aina ya Masiha,wakulima wa Kishapu wanachangamoto ya mazao yao kushambiliwa na ndege hao ambao inasemekana wanakula zaidi ya gunia 5 kwa siku hali ambayo inatishia njaa katika wilaya hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post