MAMLAKA YA MAPATO NCHINI (TRA) YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA KUHUSU MASHINE ZA EFDs

Awali meneja wa TRA mkoa wa Shinyanga  Ernest Dundee akifungua mafunzo hayo ya siku moja kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga katika ukumbi wa Karena Hoteli mjini Shinyanga alisema vyombo vya habari ni kiunganishi muhimu kati ya TRA na wananchi ndiyo maaana wameandaa mafunzo kwao ili kuwajengea uelewa zaidi kuhusu mashine za EFDs ili waweze kuandika habari zao kwa usahihi zaidi.
Afisa mwandamizi Mkuu Elimu TRA Makao Makuu jijini Dar es salaam Hamisi Lupenja akizungumza leo wakati wa mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Shinyanga kuhusu matumizi ya mashine za kodi za kutolea risiti (EFDS)iliyofanyika katika ukumbi wa Karena Hoteli mjini Shinyanga.

Alisema Serikali iliamua kuanzisha mfumo wa utoaji risiti kwa kutumia mashine za kodi (EFDs) 1 Julai,2010,ambapo awamu ya kwanza ni kwa wafanyabiashara waliosajiliwa na VAT  na  awamu ya pili  ni kwa wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa na VAT.
Waandishi wa habari wakifuatilia mafunzo,ambapo Afisa mwandamizi mkuu elimu TRA Makao Makuu jijini Dar es salaam Hamisi Lupenja aliongeza kuwa mfumo huo ulianza na wafanyabiashara wa VAT mwaka  Julai, 2010 na mfumo wa pili ulizinduliwa 15/5/2014 na unahusu wale ambao hawajasajiliwa na VAT wenye mauzo yanayozidi milioni 14.0 kwa mwaka na unaanza na wafanyabiashara 200,000.

Lupenja ambaye alikuwa mwezeshaji aliongeza kuwa pamoja mashine hizo kuwa na faida  kama vile kutoa uhakika wa usalama wa taarifa za biashara kwani taarifa hizo hutunzwa katika kifaa maalumu(Fiscal memory) pia ni njia nzuri ya kupunguza ujanja na wizi unaoweza kufanywa na wauzaji ambao si wenye mali lakini bado wafanyabiashara hawatumii mashine hizo kwa sababu mbalimbali.

Aliyesimama ni bwana Chibura Makorongo wa gazeti la Uhuru na Mzalendo akichangia mawili matatu katika mafunzo hayo kwa waandishi wa habari.Katika mafunzo hayo mwezeshaji Lupenja aliziomba taasisi zote kufanya manunuzi kwa wafanyabiashara wenye mashine za EFDs pamoja wananchi kujenga tabia ya kudai risiti ili kuwa na uhakika na uhalali wa bidhaa zilizonunuliwa na kuonyesha uzalendo kwa kuchangia katika maendeleo ya taifa.

Mwezeshaji huyo alitumia fursa hiyo pia kubainisha aina tatu za mashine za kodi Rejesta za Kodi za Kielekitroniki (Electronic Tax Register - ETR) ambapo Rejesta hii hutumika kwa wafanyabiashara wa rejareja, wanaotoa risiti kwa maandishi ya mkono na wale ambao watakuwa wanauza bidhaa kwa kutembeza kwa wateja.

Alitaja aina ya pili ni Printa za kosi za kielektroniki za Kodi (Electronic Fiscal Printer EFP) ambapo alisema Mashine hii hutumika kwa wafanyabiashara wa rejareja ambao wanatumia mtandao wa kompyuta katika utoaji wa risiti na ankara za madai na kwamba mashine hii hutumika hususani katika   maduka makubwa (Supermarkets), Vituo vya   Mafuta (Petrol Stations) na shughuli za ukataji wa risiti (Ticketing).

Alisema aina ya tatu ni Mashine za Alama za      Kodi (Electronic Signature Devise - ESD) ambapo alisema mashine hizi hutumika kwa wafanyabiashara ambao hutumia programu maalumu za biashara katika utoaji wa risiti na ankara za madai na kwamba Mashine hizi zina uwezo wa kuratibu shughuli za kibiashara katika mtandao huo na kuifanya kompyuta kutokuwa na uwezo wa kutunza (save) au kuchapa (print) taarifa yoyoye bila idhini ya mashine yenyewe. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post