JESHI LA ZIMAMOTO KAHAMA LAFANYIA KAZI MAKABURINI

Katika hali ya kushangaza  Jeshi la Zimamoto la Halmashauri ya Mji wa Kahama limekosa ofisi ya kufanyia kazi hivyo kulazimika kuhamishia ofisi katika eneo ambalo linasadikiwa kuwa lilikuwa na makaburi hapo awali.

Jeshi hilo ambalo ni muhimu katika matika matukio ya uzimaji wa moto katika Mji wa Kahama pia wamejikuta wakikosa ofisi za kufanyia kazi hali ambayo imewafanya kufanyia shughuli zao za kiofisi katika gari lao la kuzimia moto.

Baadhi ya watumishi wa Jeshi hilo wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kuhusu kupatiwa eneo la kufanyia kazi lakini jitihada zao zimekuwa zikigonga mwamba huku wakiendelea kusota katika mazingira magumu ya kufanyia kazi

Akiongea na mwandishi wa habari hizi juzi Mkaguzi wa Jeshi hilo Mkoa wa Shinyanga Rashidi Mwinyimkuu alisema madai hayo yanayodai askari wa jeshi la zimamoto ni ya msingi na kuongeza kuwa wamekuwa wakijitahidi kupata eneo la kufanyia kazi lakini mazungumzo bado yanaendeleo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala.

“Unajua ndugu Mwandishi Jeshi la zimamoto katika Halmashauri ya Mji wa Kahama limeanzishwa hivi karibuni baada ya kuzaliwa kwa Halmashari hiyo na kwa sasa tupo katika mkakati mkubwa wa kuhakikisha kuwa tunapata maeneo kwa ajili ya kufanyia kazi askari hawa”, Alisema Rashidi Mwinyimkuu.

Pia Mkaguzi huyo aliendelea kusema kuwa kwa sasa wananchi wa Mji wa Kahama wanahitaji kupata elimu kubwa juu ya matukio yanayohusu moto ikiwa ni sambamba na kutumia vifaa maalumu vya kuzimia moto katika maeneo mbalimbali ya maduka mahotel na sehemu nyingine.

Alisema wilaya ya Kahama kwa sasa inakuwa kwa haraka zaidi na watu wakiendelea kujenga nyumba nyingi ikiwa ni pamoja na maeneo ya biashara kuwa mengi hivyo lazima kuwepo na ofisi ya zimamoto katikati ya mji  ambayo itasadia wa kiasi kikubwa kuwahi matukio.

Hata hivyo Mkaguzi huyo alisema kuwa Changamoto nyingine inayoikabili ofisi yake ya zimamoto ni pamoja na kutokuwa na namba maalumu kwa ajili ya Wananchi kupiga pindi matukio ya moto yanapotokea na kuongeza kuwa hali hiyo inatokana na kutokuwa na ofisi maalumu kwa ajili ya kufanyia kazi.

via>>mihayorj blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post