SASA, NI MARUFUKU KUCHUMBIA MAZAO SHAMBANI

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza amepiga marufuku mtindo wa kuchumbia mazao shambani akisema kufanya hivyo ni kumnyima mkulima kipato anachostahili.
Alisema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akikagua eneo linalotarajiwa kujengwa soko la kimataifa huko Njiapanda Himo, mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na wafanyabiashara wa eneo hilo, Chiza alisema ni marufuku kwa mtu yeyote kuchumbia mazao yakiwa shambani kwani inawezekana mazao hayo yakazidi kiwango cha fedha alizopewa.
Aidha, alisema mtindo huo unainyima Serikali mapato kwani baadhi wanapovuna hupitisha njia za panya.
Waziri Chiza alisema hayo baada ya mfanyabiashara, Gabriel Emmanuel anayefanya shughuli zake katika Ghala la Himo linalohifadhi mahindi na maharagwe kumlalamikia kuwa wafanyabiashara kutoka Kenya wanawazidi kete.
Alimweleza waziri kuwa wafanyabiashara hao wananunua mazao kwa wanavijiji kabla hayajavunwa.
Waziri aliupongeza uongozi wa Wilaya ya Rombo hususan eneo la Tarakea kwa ukusanyaji wa mapato ambao alisema umepanda kutoka Sh2 milioni hadi kufikia Sh4.5 milioni mwaka huu.
Na Na Hussein Nyari-Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post